1
1 Wakorintho 15:58
Neno: Bibilia Takatifu
Kwa hiyo, ndugu zangu wapenzi, simameni imara, msitikisike, mzidi sana katika kuitenda kazi ya Bwana, kwa maana mnajua ya kuwa, kazi yenu katika Bwana si bure.
Compare
Explore 1 Wakorintho 15:58
2
1 Wakorintho 15:57
Lakini ashukuriwe Mungu, yeye atupaye ushindi kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Explore 1 Wakorintho 15:57
3
1 Wakorintho 15:33
Msidanganyike: “Ushirika na watu wabaya huharibu tabia njema.”
Explore 1 Wakorintho 15:33
4
1 Wakorintho 15:10
Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa hivi nilivyo na neema yake kwangu haikuwa kitu bure. Bali nilizidi sana kufanya kazi kuliko mitume wote, lakini haikuwa mimi, bali ni ile neema ya Mungu iliyokuwa pamoja nami.
Explore 1 Wakorintho 15:10
5
1 Wakorintho 15:55-56
“Kuko wapi, ee mauti, kushinda kwako? Uko wapi, ee mauti, uchungu wako?” Uchungu wa mauti ni dhambi na nguvu ya dhambi ni sheria.
Explore 1 Wakorintho 15:55-56
6
1 Wakorintho 15:51-52
Sikilizeni, nawaambia siri: Sote hatutalala, lakini sote tutabadilishwa ghafula, kufumba na kufumbua, parapanda ya mwisho itakapolia. Kwa kuwa parapanda italia, nao wafu watafufuliwa na miili isiyoharibika, nasi tutabadilishwa.
Explore 1 Wakorintho 15:51-52
7
1 Wakorintho 15:21-22
Kwa maana kama vile mauti ilivyokuja kwa njia ya mtu mmoja, vivyo hivyo, ufufuo wa wafu umekuja kwa njia ya mtu mmoja. Kwa maana kama vile katika Adamu watu wote wanakufa, vivyo hivyo katika Kristo wote watafanywa hai.
Explore 1 Wakorintho 15:21-22
8
1 Wakorintho 15:53
Kwa maana mwili huu wa kuharibika lazima uvae kutokuharibika, nao huu wa kufa lazima uvae kutokufa.
Explore 1 Wakorintho 15:53
9
1 Wakorintho 15:25-26
Kwa maana lazima Kristo atawale mpaka awe amewaweka adui zake wote chini ya miguu yake. Adui wa mwisho atakayeangamizwa ni mauti.
Explore 1 Wakorintho 15:25-26
Home
Bible
Plans
Videos