1
1 Petro 3:15-16
Neno: Bibilia Takatifu
Bali mtakaseni Kristo kuwa Bwana mioyoni mwenu. Siku zote mwe tayari kumjibu mtu yeyote atakayewauliza kuhusu sababu ya tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa heshima, mkizitunza dhamiri zenu ziwe safi, ili wale wasemao mabaya dhidi ya mwenendo wenu mzuri katika Kristo waaibike kwa ajili ya masingizio yao.
Compare
Explore 1 Petro 3:15-16
2
1 Petro 3:12
Kwa maana macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake yako makini kusikiliza maombi yao. Bali uso wa Bwana uko kinyume na watendao maovu.”
Explore 1 Petro 3:12
3
1 Petro 3:3-4
Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje tu, kama vile kusuka nywele, kuvalia vitu vilivyofanyizwa kwa dhahabu na kwa mavazi. Badala yake, kujipamba kwenu kuwe katika utu wenu wa moyoni, yaani uzuri usioharibika wa roho ya upole na utulivu, ambayo ni ya thamani sana machoni pa Mungu.
Explore 1 Petro 3:3-4
4
1 Petro 3:10-11
Kwa maana, “Yeyote apendaye uzima na kuona siku njema, basi auzuie ulimi wake usinene mabaya, na midomo yake isiseme hila. Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema; lazima aitafute amani na kuifuatilia sana.
Explore 1 Petro 3:10-11
5
1 Petro 3:8-9
Hatimaye, ninyi nyote kuweni na nia moja, wenye kuhurumiana, mkipendana kama ndugu, na mwe wasikitivu na wanyenyekevu. Msilipe ovu kwa ovu, au jeuri kwa jeuri, bali barikini, kwa maana hili ndilo mliloitiwa ili mpate kurithi baraka.
Explore 1 Petro 3:8-9
6
1 Petro 3:13
Basi, ni nani atakayewadhuru mkiwa wenye juhudi katika kutenda mema?
Explore 1 Petro 3:13
7
1 Petro 3:11
Mtu huyo lazima aache uovu, akatende mema; lazima aitafute amani na kuifuatilia sana.
Explore 1 Petro 3:11
8
1 Petro 3:17
Kwa maana ni afadhali kupata mateso kwa ajili ya kutenda mema, kama kuteseka huko ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kuteseka kwa kutenda maovu.
Explore 1 Petro 3:17
Home
Bible
Plans
Videos