1
Ezekieli 18:32
Neno: Bibilia Takatifu
Kwa maana sifurahii kifo cha mtu awaye yote afaye katika uovu, asema BWANA Mwenyezi. Tubuni basi, mkaishi!
Compare
Explore Ezekieli 18:32
2
Ezekieli 18:20
Roho itendayo dhambi ndiyo itakayokufa. Mwana hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya baba yake, wala baba hataadhibiwa kwa ajili ya makosa ya mwanawe. Haki ya mtu mwenye haki itahesabiwa juu yake na uovu wa mtu mwovu utalipizwa juu yake.
Explore Ezekieli 18:20
3
Ezekieli 18:31
Tupilieni mbali makosa yenu yote mliyoyatenda, nanyi mpate moyo mpya na roho mpya. Kwa nini mfe, ee nyumba ya Israeli?
Explore Ezekieli 18:31
4
Ezekieli 18:23
Je, mimi ninafurahia kifo cha mtu mwovu? Asema BWANA Mwenyezi. Je, si mimi ninafurahi wanapogeuka kutoka njia zao mbaya na kuishi?
Explore Ezekieli 18:23
5
Ezekieli 18:21
“Lakini mtu mwovu akiacha dhambi zake zote alizozitenda na kushika amri zangu zote na kufanya lililo haki na sawa, hakika ataishi, hatakufa.
Explore Ezekieli 18:21
6
Ezekieli 18:9
Huzifuata amri zangu na kuzishika sheria zangu kwa uaminifu. Huyo mtu ni mwenye haki; hakika ataishi, asema BWANA Mwenyezi.
Explore Ezekieli 18:9
Home
Bible
Plans
Videos