Ni nani aliyepima maji ya bahari
kwenye konzi ya mkono wake,
au kuzipima mbingu kwa shibiri yake?
Ni nani aliyeyashika mavumbi ya dunia katika kikapu,
au kupima milima kwenye kipimio
na vilima kwenye mizani?
Ni nani aliyeyafahamu mawazo ya BWANA,
au kumfundisha akiwa kama mshauri wake?
Ni nani ambaye BWANA ametaka shauri kwake ili kumwelimisha,
naye ni nani aliyemfundisha njia iliyo sawa?
Ni nani aliyemfundisha maarifa
au kumwonyesha mapito ya ufahamu?