1
Isaya 54:17
Neno: Bibilia Takatifu
Hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako itakayofanikiwa, nawe utauthibitisha kuwa mwongo kila ulimi utakaokushtaki. Huu ndio urithi wa watumishi wa BWANA na hii ndiyo haki yao itokayo kwangu,” asema BWANA.
Compare
Explore Isaya 54:17
2
Isaya 54:10
Ijapotikisika milima, na vilima viondolewe, hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika, wala agano langu la amani halitaondolewa,” asema BWANA, mwenye huruma juu yenu.
Explore Isaya 54:10
3
Isaya 54:4
“Usiogope, wewe hutaaibika. Usiogope aibu, wewe hutaaibishwa. Wewe utasahau aibu ya ujana wako, wala hutakumbuka tena mashutumu ya ujane wako.
Explore Isaya 54:4
4
Isaya 54:5
Kwa maana Muumba wako ndiye mume wako, BWANA Mwenye Nguvu Zote ndilo jina lake, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ni Mkombozi wako, yeye anaitwa Mungu wa dunia yote.
Explore Isaya 54:5
5
Isaya 54:2
“Panua mahali pa hema lako, tandaza mapazia ya hema lako uyaeneze mbali, wala usiyazuie; ongeza urefu wa kamba zako, imarisha vigingi vyako.
Explore Isaya 54:2
6
Isaya 54:13
Watoto wako wote watafundishwa na BWANA, nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu.
Explore Isaya 54:13
7
Isaya 54:8
Katika ukali wa hasira nilikuficha uso wangu kwa kitambo, lakini kwa fadhili za milele nitakuwa na huruma juu yako,” asema BWANA Mkombozi wako.
Explore Isaya 54:8
8
Isaya 54:7
“Kwa kitambo kidogo nilikuacha, lakini kwa huruma nyingi nitakurudisha.
Explore Isaya 54:7
9
Isaya 54:9
“Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Noa, nilipoapa kuwa maji ya Noa kamwe hayatafunika tena dunia. Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi, kamwe sitawakemea tena.
Explore Isaya 54:9
10
Isaya 54:12
Nitafanya minara yako ya akiki, malango yako kwa vito vingʼaavyo, nazo kuta zako zote za vito vya thamani.
Explore Isaya 54:12
Home
Bible
Plans
Videos