1
Isaya 54:17
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Hakuna silaha itakayofanyizwa dhidi yako itakayofanikiwa, nawe utauthibitisha kuwa mwongo kila ulimi utakaokushtaki. Huu ndio urithi wa watumishi wa Mwenyezi Mungu na hii ndiyo haki yao inayotoka kwangu,” asema Mwenyezi Mungu.
Compare
Explore Isaya 54:17
2
Isaya 54:10
Ijapotikisika milima, na vilima viondolewe, hata hivyo upendo wangu usiokoma kwenu hautatikisika, wala agano langu la amani halitaondolewa,” asema Mwenyezi Mungu, mwenye huruma juu yenu.
Explore Isaya 54:10
3
Isaya 54:4
“Usiogope, wewe hutaaibika. Usiogope aibu, wewe hutaaibishwa. Wewe utasahau aibu ya ujana wako, wala hutakumbuka tena mashutumu ya ujane wako.
Explore Isaya 54:4
4
Isaya 54:5
Kwa maana Muumba wako ndiye mume wako, Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni ndilo jina lake, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli ni Mkombozi wako, yeye anaitwa Mungu wa dunia yote.
Explore Isaya 54:5
5
Isaya 54:2
“Panua mahali pa hema lako, tandaza mapazia ya hema lako uyaeneze mbali, wala usiyazuie; ongeza urefu wa kamba zako, imarisha vigingi vyako.
Explore Isaya 54:2
6
Isaya 54:13
Watoto wako wote watafundishwa na Mwenyezi Mungu, nayo amani ya watoto wako itakuwa kuu.
Explore Isaya 54:13
7
Isaya 54:8
Katika ukali wa hasira nilikuficha uso wangu kwa kitambo, lakini kwa fadhili za milele nitakuwa na huruma juu yako,” asema Mwenyezi Mungu Mkombozi wako.
Explore Isaya 54:8
8
Isaya 54:7
“Kwa kitambo kidogo nilikuacha, lakini kwa huruma nyingi nitakurudisha.
Explore Isaya 54:7
9
Isaya 54:9
“Kwangu mimi jambo hili ni kama siku za Nuhu, nilipoapa kuwa maji ya Nuhu kamwe hayatafunika tena dunia. Hivyo sasa nimeapa sitawakasirikia ninyi, kamwe sitawakemea tena.
Explore Isaya 54:9
10
Isaya 54:12
Nitafanya minara yako ya akiki, malango yako kwa vito ving’aavyo, nazo kuta zako zote za vito vya thamani.
Explore Isaya 54:12
Home
Bible
Plans
Videos