1
Yakobo 3:17
Neno: Bibilia Takatifu
Lakini hekima itokayo mbinguni kwanza ni safi, kisha inapenda amani, tena ni ya upole, iliyo tayari kusikiliza wengine kwa unyenyekevu, iliyojaa huruma na matunda mema, isiyopendelea mtu, tena isiyokuwa na unafiki.
Compare
Explore Yakobo 3:17
2
Yakobo 3:13
Ni nani aliye na hekima na ufahamu miongoni mwenu? Basi na aionyeshe hiyo kwa maisha yake mema na kwa matendo yake yaliyotendwa kwa unyenyekevu utokanao na hekima.
Explore Yakobo 3:13
3
Yakobo 3:18
Mavuno ya haki hupandwa katika amani na wale wafanyao amani.
Explore Yakobo 3:18
4
Yakobo 3:16
Kwa maana panapokuwa na wivu na ubinafsi, ndipo penye machafuko na uovu wa kila namna.
Explore Yakobo 3:16
5
Yakobo 3:9-10
Kwa ulimi tunamhimidi Bwana, yaani Baba yetu, na kwa huo twawalaani watu walioumbwa kwa mfano wa Mungu. Katika kinywa kile kile hutoka baraka na laana. Ndugu zangu, haistahili kuwa hivyo.
Explore Yakobo 3:9-10
6
Yakobo 3:6
Ulimi pia ni moto, ndio ulimwengu wa uovu kati ya viungo vya mwili. Ulimi huutia mwili wote wa mtu unajisi na kuuwasha moto mfumo mzima wa maisha yake, nao wenyewe huchomwa moto wa jehanamu.
Explore Yakobo 3:6
7
Yakobo 3:8
lakini hakuna mtu awezaye kuufuga ulimi. Ni uovu usiotulia, umejaa sumu iletayo mauti.
Explore Yakobo 3:8
8
Yakobo 3:1
Ndugu zangu, msiwe walimu wengi, kwa maana mnafahamu kwamba sisi tufundishao tutahukumiwa vikali zaidi.
Explore Yakobo 3:1
Home
Bible
Plans
Videos