1
Yoshua 1:9
Neno: Bibilia Takatifu
Je, si mimi niliyekuamuru? Uwe hodari na shujaa. Usihofu wala usivunjike moyo, kwa kuwa BWANA Mungu wako atakuwa pamoja nawe kokote uendako.”
Compare
Explore Yoshua 1:9
2
Yoshua 1:8
Usiache Kitabu hiki cha Sheria kiondoke kinywani mwako; yatafakari maneno yake usiku na mchana, ili upate kuwa mwangalifu kufanya kila kitu sawasawa na yote yaliyoandikwa ndani yake. Ndipo utakapofanikiwa na kisha utastawi.
Explore Yoshua 1:8
3
Yoshua 1:7
Uwe hodari na uwe na ushujaa mwingi. Uwe na bidii kutii sheria yote aliyokupa Mose mtumishi wangu, usiiache kwa kugeuka kuelekea kuume au kushoto, ili upate kufanikiwa popote uendako.
Explore Yoshua 1:7
4
Yoshua 1:5
Hakuna mtu yeyote atakayeweza kushindana na wewe siku zote za maisha yako. Kama vile nilivyokuwa pamoja na Mose, ndivyo nitakavyokuwa pamoja na wewe, sitakuacha wala sitakupungukia.
Explore Yoshua 1:5
5
Yoshua 1:6
“Uwe hodari na shujaa, kwa sababu wewe ndiwe utakayewaongoza watu hawa kuirithi nchi niliyowaapia baba zao kuwapa.
Explore Yoshua 1:6
6
Yoshua 1:3
Kila mahali nyayo za miguu yenu zitakapokanyaga nimewapa, kama vile nilivyomwahidi Mose.
Explore Yoshua 1:3
7
Yoshua 1:2
“Mtumishi wangu Mose amekufa. Sasa basi, wewe pamoja na watu wote hawa, jiandaeni kuvuka huu Mto Yordani kuingia nchi ambayo karibu nitawapa wana wa Israeli.
Explore Yoshua 1:2
8
Yoshua 1:1
Baada ya kifo cha Mose mtumishi wa BWANA, BWANA akamwambia Yoshua mwana wa Nuni, msaidizi wa Mose
Explore Yoshua 1:1
9
Yoshua 1:4
Nchi yenu itaenea kuanzia jangwa hili hadi Lebanoni, tena kuanzia mto mkubwa wa Frati, yaani nchi yote ya Wahiti, hadi Bahari ile Kubwa iliyoko upande wa magharibi.
Explore Yoshua 1:4
10
Yoshua 1:18
Yeyote atakayeasi neno lako na kuacha kuyatii maneno yako, au chochote utakachowaamuru, atauawa. Uwe imara na hodari tu!”
Explore Yoshua 1:18
11
Yoshua 1:11
“Pitieni katika kambi yote mkawaambie watu, ‘Wekeni tayari mahitaji yenu. Siku tatu kuanzia sasa mtavuka hii Yordani ili kuingia na kuimiliki nchi ambayo BWANA Mungu wenu anawapa iwe yenu wenyewe.’ ”
Explore Yoshua 1:11
Home
Bible
Plans
Videos