1
Walawi 26:12
Neno: Bibilia Takatifu
Nitatembea katikati yenu niwe Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.
Compare
Explore Walawi 26:12
2
Walawi 26:4
nitawanyeshea mvua katika majira yake, nayo ardhi itatoa mazao yake, na miti ya mashambani itazaa matunda yake.
Explore Walawi 26:4
3
Walawi 26:3
“ ‘Ikiwa mtafuata amri zangu na kuwa waangalifu kutii maagizo yangu
Explore Walawi 26:3
4
Walawi 26:6
“ ‘Nitawapa amani katika nchi, mpate kulala pasipo kutiwa hofu na yeyote. Nitawaondoa wanyama wakali watoke kwenye nchi, nao upanga hautapita katika nchi yenu.
Explore Walawi 26:6
5
Walawi 26:9
“ ‘Nitawaangalia kwa upendeleo na kuwafanya mzae na kuzidisha idadi yenu, nami nitalishika Agano langu na ninyi.
Explore Walawi 26:9
6
Walawi 26:13
Mimi ndimi BWANA Mungu wenu, niliyewatoa katika nchi ya Misri ili msiendelee kuwa watumwa wa Wamisri, nikavunja kongwa lenu, na kuwawezesha kutembea mkiwa mmeinua vichwa vyenu juu.
Explore Walawi 26:13
7
Walawi 26:11
Nitafanya makao yangu miongoni mwenu, nami sitawachukia.
Explore Walawi 26:11
8
Walawi 26:1
“ ‘Msijitengenezee sanamu au kusimamisha kinyago cha kuchonga, au mnara, wala jiwe la kuabudia, na pia msijiwekee jiwe lililochongwa katika nchi yenu na kusujudu mbele yake. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu.
Explore Walawi 26:1
9
Walawi 26:10
Wakati wa kuvuna mtakuwa bado mnakula mavuno ya mwaka uliopita, na itawalazimu kuyaondoa ghalani ili mpate nafasi ya mavuno mapya.
Explore Walawi 26:10
10
Walawi 26:8
Watu wenu watano watafukuza adui mia, watu wenu mia watafukuza adui elfu kumi, nao adui zenu wataanguka kwa upanga mbele yenu.
Explore Walawi 26:8
11
Walawi 26:5
Kupura nafaka kwenu kutaendelea mpaka wakati wa kuvuna zabibu. Pia kuvuna zabibu kutaendelea mpaka wakati wa kupanda mbegu, nanyi mtakula na kushiba, na mtaishi salama katika nchi yenu.
Explore Walawi 26:5
12
Walawi 26:7
Mtawafukuza adui zenu, nanyi mtawaua kwa upanga mbele yenu.
Explore Walawi 26:7
13
Walawi 26:2
“ ‘Zishikeni Sabato zangu na kuheshimu mahali patakatifu pangu. Mimi ndimi BWANA.
Explore Walawi 26:2
Home
Bible
Plans
Videos