1
Marko 4:39-40
Neno: Bibilia Takatifu
Akaamka, akaukemea ule upepo, akayaambia yale mawimbi, “Uwe kimya! Tulia!” Ule upepo ukatulia, kukawa shwari kabisa. Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Kwa nini mnaogopa hivyo? Je, bado hamna imani?”
Compare
Explore Marko 4:39-40
2
Marko 4:41
Nao wakawa wameogopa sana, wakaulizana, “Ni nani huyu ambaye hata upepo na mawimbi vinamtii?”
Explore Marko 4:41
3
Marko 4:38
Yesu alikuwa katika shetri, akiwa analala juu ya mto. Wanafunzi wake wakamwamsha, wakamwambia, “Mwalimu, hujali kama tunazama?”
Explore Marko 4:38
4
Marko 4:24
Naye akawaambia, “Kuweni waangalifu na yale mnayosikia. Kipimo kile mpimacho, ndicho mtakachopimiwa ninyi, hata na zaidi.
Explore Marko 4:24
5
Marko 4:26-27
Pia akawaambia, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu apandaye mbegu shambani. Akiisha kuzipanda, usiku na mchana, akiwa amelala au ameamka, mbegu huota na kukua pasipo yeye kujua ikuavyo.
Explore Marko 4:26-27
6
Marko 4:23
Mwenye masikio ya kusikia, na asikie.”
Explore Marko 4:23
Home
Bible
Plans
Videos