1
Ufunuo 2:4
Neno: Bibilia Takatifu
“Lakini nina neno dhidi yako: Umeuacha upendo wako wa kwanza.
Compare
Explore Ufunuo 2:4
2
Ufunuo 2:5
Kumbuka basi ni wapi ulikoangukia! Tubu na ukafanye matendo yale ya kwanza. Kama usipotubu, nitakuja kwako na kukiondoa kinara chako cha taa kutoka mahali pake.
Explore Ufunuo 2:5
3
Ufunuo 2:10
Usiogope mateso yatakayokupata. Nakuambia ibilisi atawatia baadhi yenu gerezani ili kuwajaribu, nanyi mtapata dhiki kwa muda wa siku kumi. Uwe mwaminifu hata kufa, nami nitakupa taji ya uzima.
Explore Ufunuo 2:10
4
Ufunuo 2:7
“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye, nitampa haki ya kula matunda toka kwa mti wa uzima, ambao uko katika paradiso ya Mungu.
Explore Ufunuo 2:7
5
Ufunuo 2:2
Nayajua matendo yako, bidii yako na saburi yako. Najua kuwa huwezi kuvumiliana na watu waovu na ya kwamba umewajaribu wale wanaojifanya kuwa mitume na kumbe sio, nawe umewatambua kuwa ni waongo.
Explore Ufunuo 2:2
6
Ufunuo 2:3
Umevumilia na kustahimili taabu kwa ajili ya Jina langu, wala hukuchoka.
Explore Ufunuo 2:3
7
Ufunuo 2:17
“Yeye aliye na sikio na asikie yale ambayo Roho ayaambia makanisa. Yeye ashindaye nitampa baadhi ya ile mana iliyofichwa. Nitampa pia jiwe jeupe ambalo juu yake limeandikwa jina jipya asilolijua mtu, isipokuwa yule anayelipokea.
Explore Ufunuo 2:17
Home
Bible
Plans
Videos