1
Warumi 2:3-4
Neno: Bibilia Takatifu
Hivyo wewe mwanadamu, utoapo hukumu juu yao na bado unafanya mambo yale yale, unadhani utaepuka hukumu ya Mungu? Au waudharau wingi wa wema, ustahimili na uvumilivu wake, bila kujua kuwa wema wa Mungu wakuelekeza kwenye toba?
Compare
Explore Warumi 2:3-4
2
Warumi 2:1
Kwa hiyo huna udhuru wowote, wewe utoaye hukumu kwa mwingine, kwa maana katika jambo lolote unalowahukumu wengine, unajihukumu wewe mwenyewe kwa sababu wewe unayehukumu unafanya mambo hayo hayo.
Explore Warumi 2:1
3
Warumi 2:11
Kwa maana Mungu hana upendeleo.
Explore Warumi 2:11
4
Warumi 2:13
Kwa maana si wale wanaoisikia sheria ambao ni wenye haki mbele za Mungu, bali ni wale wanaoitii sheria ndio watakaohesabiwa haki.
Explore Warumi 2:13
5
Warumi 2:6
Kwa maana Mungu atamlipa kila mtu sawasawa na matendo yake.
Explore Warumi 2:6
6
Warumi 2:8
Lakini kwa wale watafutao mambo yao wenyewe na wale wanaokataa kweli na kuzifuata njia mbaya, kutakuwa na ghadhabu na hasira ya Mungu.
Explore Warumi 2:8
7
Warumi 2:5
Lakini kwa sababu ya ukaidi wenu na mioyo yenu isiyotaka kutubu, mnajiwekea akiba ya ghadhabu dhidi yenu wenyewe kwa siku ile ya ghadhabu ya Mungu, wakati hukumu yake ya haki itakapodhihirishwa.
Explore Warumi 2:5
Home
Bible
Plans
Videos