1
Tito 2:11-12
Neno: Maandiko Matakatifu 2024
Kwa maana neema ya Mungu ambayo inawaokoa wanadamu wote imefunuliwa. Nayo inatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ili tupate kuishi maisha ya kiasi, ya haki na ya utaua katika ulimwengu huu wa sasa
Compare
Explore Tito 2:11-12
2
Tito 2:13-14
huku tukilitazamia tumaini lenye baraka na ufunuo wa utukufu wa Mungu wetu Mkuu, aliye Mwokozi wetu Isa Al-Masihi. Ndiye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe kutoka uovu wote na kujisafishia watu kuwa mali yake Mwenyewe, yaani wale walio na juhudi katika kutenda mema.
Explore Tito 2:13-14
3
Tito 2:7-8
Katika kila jambo uwe kielelezo kwa kutenda mema. Katika mafundisho yako uoneshe uadilifu, utaratibu, na usemi sahihi usio na lawama, ili wanaokupinga watahayari, wakose neno lolote baya la kusema kutuhusu.
Explore Tito 2:7-8
Home
Bible
Plans
Videos