1
Kum 4:29
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
Lakini huko, kama mkimtafuta BWANA, Mungu wako, utampata, ukimtafuta kwa moyo wako wote, na roho yako yote.
Compare
Explore Kum 4:29
2
Kum 4:31
kwa kuwa BWANA, Mungu wako, ni Mungu wa rehema; hatakukosa wala kukuangamiza, wala hatalisahau agano la baba zako alilowaapia.
Explore Kum 4:31
3
Kum 4:24
kwa kuwa BWANA, Mungu wenu, ni moto ulao, Mungu mwenye wivu.
Explore Kum 4:24
4
Kum 4:9
Lakini, jihadhari nafsi yako, ukailinde roho yako kwa bidii, usije ukayasahau mambo yale uliyoyaona kwa macho yako, yakaondoka moyoni mwako siku zote za maisha yako; bali uwajulishe watoto wako na watoto wa watoto wako
Explore Kum 4:9
5
Kum 4:39
Kwa hiyo ujue, leo hivi, ukaweke moyoni mwako, ya kuwa BWANA ndiye Mungu katika mbingu juu, na katika nchi chini; hapana mwingine.
Explore Kum 4:39
6
Kum 4:7
Kwa maana liko taifa gani kubwa, lililo na Mungu aliye karibu nao, kama BWANA, Mungu wetu, alivyo, kila tumwitapo?
Explore Kum 4:7
7
Kum 4:30
Na wakati uwapo katika mashaka, ukiisha kupatwa na mambo haya yote, siku za mwisho, utamrudia BWANA, Mungu wako, na kuisikiza sauti yake
Explore Kum 4:30
8
Kum 4:2
Msiliongeze neno niwaamurulo wala msilipunguze, mpate kuzishika amri za BWANA, Mungu wenu, niwaamuruzo.
Explore Kum 4:2
Home
Bible
Plans
Videos