1
Mt 7:7
Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia
Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa
Compare
Explore Mt 7:7
2
Mt 7:8
kwa maana kila aombaye hupokea; naye atafutaye huona; naye abishaye atafunguliwa.
Explore Mt 7:8
3
Mt 7:24
Basi kila asikiaye hayo maneno yangu, na kuyafanya, atafananishwa na mtu mwenye akili, aliyejenga nyumba yake juu ya mwamba
Explore Mt 7:24
4
Mt 7:12
Basi yo yote myatakayo mtendewe na watu, nanyi watendeeni vivyo hivyo; maana hiyo ndiyo torati na manabii.
Explore Mt 7:12
5
Mt 7:14
Bali mlango ni mwembamba, na njia imesonga iendayo uzimani, nao waionao ni wachache.
Explore Mt 7:14
6
Mt 7:13
Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
Explore Mt 7:13
7
Mt 7:11
Basi ikiwa ninyi, mlio waovu, mnajua kuwapa watoto wenu vipawa vyema, je! Si zaidi sana Baba yenu aliye mbinguni atawapa mema wao wamwombao?
Explore Mt 7:11
8
Mt 7:1-2
Msihukumu, msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu ile mhukumuyo, ndiyo mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa.
Explore Mt 7:1-2
9
Mt 7:26
Na kila asikiaye hayo maneno yangu asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu, aliyejenga nyumba yake juu ya mchanga
Explore Mt 7:26
10
Mt 7:3-4
Basi, mbona wakitazama kibanzi kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho lako mwenyewe?
Explore Mt 7:3-4
11
Mt 7:15-16
Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti?
Explore Mt 7:15-16
12
Mt 7:17
Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya.
Explore Mt 7:17
13
Mt 7:18
Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri.
Explore Mt 7:18
14
Mt 7:19
Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni.
Explore Mt 7:19
Home
Bible
Plans
Videos