1
Yohana 14:27
Swahili Revised Union Version
Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga.
Compare
Explore Yohana 14:27
2
Yohana 14:6
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Explore Yohana 14:6
3
Yohana 14:1
Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi.
Explore Yohana 14:1
4
Yohana 14:26
Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.
Explore Yohana 14:26
5
Yohana 14:21
Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu; nami nitampenda na kujidhihirisha kwake.
Explore Yohana 14:21
6
Yohana 14:16-17
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; ndiye Roho wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.
Explore Yohana 14:16-17
7
Yohana 14:13-14
Nanyi mkiomba lolote kwa jina langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba neno lolote kwa jina langu, nitalifanya.
Explore Yohana 14:13-14
8
Yohana 14:15
Mkinipenda, mtazishika amri zangu.
Explore Yohana 14:15
9
Yohana 14:2
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
Explore Yohana 14:2
10
Yohana 14:3
Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi muwepo.
Explore Yohana 14:3
11
Yohana 14:5
Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi tunaijuaje njia?
Explore Yohana 14:5
Home
Bible
Plans
Videos