1
Yohana 19:30
Swahili Revised Union Version
Basi Yesu alipokwisha kuipokea ile siki, alisema, Imekwisha. Akainama kichwa, akaisalimu roho yake.
Compare
Explore Yohana 19:30
2
Yohana 19:28
Baada ya hayo Yesu, hali akijua ya kuwa yote yamekwisha kumalizika ili andiko litimizwe, akasema, Naona kiu.
Explore Yohana 19:28
3
Yohana 19:26-27
Basi Yesu alipomwona mama yake, na yule mwanafunzi aliyempenda amesimama karibu, alimwambia mama yake, Mama, tazama, mwanao. Kisha akamwambia yule mwanafunzi, Tazama, mama yako. Na tangu saa ile mwanafunzi yule akamchukua nyumbani kwake.
Explore Yohana 19:26-27
4
Yohana 19:33-34
Lakini walipomjia Yesu na kuona ya kuwa amekwisha kufa, hawakumvunja miguu; lakini askari mmojawapo alimchoma ubavu kwa mkuki; na mara ikatoka damu na maji.
Explore Yohana 19:33-34
5
Yohana 19:36-37
Kwa maana hayo yalitukia ili andiko litimie, Hapana mfupa wake utakaovunjwa. Na tena andiko lingine lanena, Watamtazama yeye waliyemchoma.
Explore Yohana 19:36-37
6
Yohana 19:17
Akatoka, huku akijichukulia msalaba wake, mpaka mahali paitwapo Fuvu la Kichwa, au kwa Kiebrania, Golgotha.
Explore Yohana 19:17
7
Yohana 19:2
Nao askari wakasokota taji la miiba, wakamtia kichwani, wakamvika vazi la zambarau.
Explore Yohana 19:2
Home
Bible
Plans
Videos