1
Mathayo 18:20
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Ndiyo, ikiwa watu wawili au watatu wanaoniamini watakusanyika pamoja, mimi nitakuwa pamoja nao.”
Compare
Explore Mathayo 18:20
2
Mathayo 18:19
Kwa namna nyingine, ikiwa watu wawili waliopo duniani watakubaliana kwa kila wanachokiombea, Baba yangu wa mbinguni atatenda kile wanachokiomba.
Explore Mathayo 18:19
3
Mathayo 18:2-3
Yesu akamwita mtoto mdogo, akamsimamisha mbele yao. Kisha akasema, “Ukweli ni huu, ni lazima mbadilike katika namna mnavyofikiri na muwe kama mtoto mdogo. Msipofanya hivi hamtaingia katika ufalme wa Mungu.
Explore Mathayo 18:2-3
4
Mathayo 18:4
Aliye mkuu zaidi katika ufalme wa Mungu ni yule anayejinyenyekeza kama mtoto huyu.
Explore Mathayo 18:4
5
Mathayo 18:5
Unapomkubali mtoto mdogo kama huyu kama aliye wangu, unanikubali mimi.
Explore Mathayo 18:5
6
Mathayo 18:18
Ninawahakikishia kuwa mnapotoa hukumu hapa duniani, hukumu hiyo itakuwa hukumu ya Mungu. Na mnapotoa msamaha, nao utakuwa msamaha wa Mungu.
Explore Mathayo 18:18
7
Mathayo 18:35
Mfalme huyu alifanya kama ambavyo Baba yangu wa mbinguni atawafanyia ninyi. Ni lazima umsamehe ndugu au dada yako kwa moyo wako wote, usipofanya hivyo, Baba yangu wa mbinguni hatakusamehe wewe.”
Explore Mathayo 18:35
8
Mathayo 18:6
Ikiwa mmoja wa watoto hawa wadogo ananiamini, na mtu yeyote akasababisha mtoto huyo kutenda dhambi, ole wake mtu huyo. Ingekuwa bora mtu huyo kufungiwa jiwe la kusagia shingoni mwake na kuzamishwa katika kina kirefu baharini.
Explore Mathayo 18:6
9
Mathayo 18:12
Mtu akiwa na kondoo 100, lakini mmoja wa kondoo akapotea, atafanya nini? Atawaacha kondoo wengine 99 kwenye kilima na kwenda kumtafuta mmoja aliyepotea. Sawa?
Explore Mathayo 18:12
Home
Bible
Plans
Videos