1
Mathayo 26:41
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Amkeni kesheni na kuomba ili muyashinde majaribu. Roho zenu zinataka kufanya mambo sahihi, lakini miili yenu ni dhaifu.”
Compare
Explore Mathayo 26:41
2
Mathayo 26:38
Yesu akamwambia Petro na wana wa Zebedayo, “Moyo wangu ni mzito na wenye huzuni hata kujisikia kana kwamba huzuni hiyo itaniua. Kaeni hapa mkeshe pamoja nami.”
Explore Mathayo 26:38
3
Mathayo 26:39
Kisha Yesu akaenda mbele kidogo. Akainama hadi chini uso wake ukiigusa nchi akiomba na akasema, “Baba yangu, ikiwezekana, usifanye nikinywee kikombe hiki cha mateso. Lakini fanya lile ulitakalo na si lile ninalolitaka mimi.”
Explore Mathayo 26:39
4
Mathayo 26:28
Divai hii ni damu yangu, itakayomwagika ili kusamehe dhambi za watu wengi na kuanza Agano Jipya ambalo Mungu analifanya na watu wake.
Explore Mathayo 26:28
5
Mathayo 26:26
Walipokuwa wakila, Yesu alichukua baadhi ya mikate na akamshukuru Mungu. Alimega baadhi ya vipande, akawapa wafuasi wake na akasema, “Chukueni mkate huu na mle. Ni mwili wangu.”
Explore Mathayo 26:26
6
Mathayo 26:27
Kisha akachukua kikombe chenye divai, akamshukuru Mungu na akawapa. Akasema, “Kila mmoja wenu anywe divai iliyo katika kikombe hiki.
Explore Mathayo 26:27
7
Mathayo 26:40
Kisha akarudi walipokuwa wafuasi wake na akawakuta wamelala. Akamwambia Petro, “Je hamkuwa na uwezo wa kukesha pamoja nami hata kwa saa moja?
Explore Mathayo 26:40
8
Mathayo 26:29
Ninataka mjue kuwa, hii ni mara ya mwisho nitakunywa divai mpaka siku ile nitakapokunywa divai mpya pamoja nanyi katika ufalme wa Baba yangu.”
Explore Mathayo 26:29
9
Mathayo 26:75
Kisha akakumbuka maneno alivyoambiwa na Yesu kuwa: “Kabla jogoo hajawika, utakuwa umenikana mara tatu.” Kisha Petro akatoka nje na kulia kwa uchungu sana.
Explore Mathayo 26:75
10
Mathayo 26:46
Simameni! Tuondoke. Tazama yeye atakayenikabidhi anakuja.”
Explore Mathayo 26:46
11
Mathayo 26:52
Yesu akamwambia, “Rudisha jambia lako mahali pake. Atumiaye jambia atauawa kwa jambia.
Explore Mathayo 26:52
Home
Bible
Plans
Videos