1
Yohana 10:10
BIBLIA KISWAHILI
Mwizi huja tu kuiba, kuua na kuharibu; mimi nilikuja ili wawe na uzima, tena wawe nao tele.
Compare
Explore Yohana 10:10
2
Yohana 10:11
Mimi ndimi mchungaji mwema. Mchungaji mwema huutoa uhai wake kwa ajili ya kondoo.
Explore Yohana 10:11
3
Yohana 10:27
Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata.
Explore Yohana 10:27
4
Yohana 10:28
Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu.
Explore Yohana 10:28
5
Yohana 10:9
Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho.
Explore Yohana 10:9
6
Yohana 10:14
Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi
Explore Yohana 10:14
7
Yohana 10:29-30
Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Mimi na Baba tu mmoja.
Explore Yohana 10:29-30
8
Yohana 10:15
kama vile Baba anijuavyo, nami nimjuavyo Baba. Nami nautoa uhai wangu kwa ajili ya kondoo.
Explore Yohana 10:15
9
Yohana 10:18
Hakuna mtu aniondoleaye, bali mimi nautoa mwenyewe. Nami ninao uweza wa kuutoa, ninao na uweza wa kuutwaa tena. Agizo hilo nililipokea kwa Baba yangu.
Explore Yohana 10:18
10
Yohana 10:7
Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo.
Explore Yohana 10:7
11
Yohana 10:12
Mtu wa mshahara, wala si mchungaji, ambaye kondoo si mali yake, humwona mbwamwitu anakuja, akawaacha kondoo na kukimbia; na mbwamwitu huwakamata na kuwatawanya.
Explore Yohana 10:12
12
Yohana 10:1
Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwizi naye ni mnyang'anyi.
Explore Yohana 10:1
Home
Bible
Plans
Videos