Farao atakapowaambia: Fanyeni kioja, niwajue, mwambie Haroni: Ikamate fimbo yako, uitupe chini mbele ya Farao, iwe nyoka! Mose na Haroni walipofika kwake Farao wakafanya hivyo, kama Bwana alivyowaagiza: Haroni alipoitupa fimbo yake chini mbele yake Farao na mbele yao watumishi wake, ikawa nyoka.