1
Yohana 14:27
Swahili Roehl Bible 1937
Nawaachia utengemano, utengemano wangu nawapani. Mimi siwapi, kama ulimwengu unavyowapa. Mioyo yenu isizizimke, wala isiogope!
Compare
Explore Yohana 14:27
2
Yohana 14:6
Yesu akamwambia: Mimi ndiyo njia na kweli na uzima; hakuna atakayefika kwa Baba asiponishika mimi.*
Explore Yohana 14:6
3
Yohana 14:1
Mioyo yenu isizizimke! Mtegemeeni Mungu, nami mnitegemee!
Explore Yohana 14:1
4
Yohana 14:26
Lakini yule mtuliza mioyo, yule Roho Mtakatifu, Baba atakayemtuma katika Jina langu, ndiye atakayewafundisha yote na kuwakumbusha yote, mimi niliyowaambia ninyi.
Explore Yohana 14:26
5
Yohana 14:21
Aliye na maagizo yangu, akiyashika, huyo ndiye mwenye kunipenda. Lakini mwenye kunipenda atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda nimwonyeshe, nilivyo.*
Explore Yohana 14:21
6
Yohana 14:16-17
Nami nitamwomba Baba, naye atawapa mtuliza mioyo mwingine, akae pamoja nanyi kale na kale. Ndiye Roho wa kweli, ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni, wala haumtambui. Ninyi mnamtambua, kwani anakaa kwenu, naye atakuwamo mwenu.
Explore Yohana 14:16-17
7
Yohana 14:13-14
Tena lo lote, mtakaloliomba katika Jina langu, nitalifanya, Baba apate kutukuzwa, kwa kuwa yumo mwake Mwana. Mtakaloniomba katika Jina langu, nitalifanya.
Explore Yohana 14:13-14
8
Yohana 14:15
*Mkinipenda yashikeni maagizo yangu!
Explore Yohana 14:15
9
Yohana 14:2
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi. Kama visingekuwa hivyo, ningewaambia: Nakwenda kuwatengenezea mahali.
Explore Yohana 14:2
10
Yohana 14:3
Nami ijapokuwa ninakwenda kuwatengenezea mahali, nitakuja tena, niwachukue kuwapeleka mwangu, kwamba nanyi mwepo hapo, nilipo mimi.
Explore Yohana 14:3
11
Yohana 14:5
Ndipo, Toma alipomwambia: Bwana, tusipopajua, unapokwenda, njia tutaijuaje?
Explore Yohana 14:5
Home
Bible
Plans
Videos