Alipofika na kuona madhihirisho ya neema ya Mwenyezi Mungu, akafurahi na kuwatia moyo waendelee kuwa waaminifu kwa Bwana Isa kwa mioyo yao yote. Barnaba alikuwa mtu mwema, aliyejaa Roho wa Mwenyezi Mungu, mwenye imani, nayo idadi kubwa ya watu wakaongezeka kwa Bwana Isa.