1
Matendo 2:38
Neno: Maandiko Matakatifu
Petro akawajibu, “Tubuni, mkabatizwe kila mmoja wenu kwa jina la Isa Al-Masihi, ili mpate kusamehewa dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho wa Mwenyezi Mungu.
Compare
Explore Matendo 2:38
2
Matendo 2:42
Nao wakawa wanadumu katika mafundisho ya mitume, katika ushirika, katika kumega mkate na katika kusali.
Explore Matendo 2:42
3
Matendo 2:4
Wote wakajazwa na Roho wa Mwenyezi Mungu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.
Explore Matendo 2:4
4
Matendo 2:2-4
Ghafula sauti kama mvumo mkubwa wa upepo mkali uliotoka mbinguni ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. Wote wakajazwa na Roho wa Mwenyezi Mungu, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia.
Explore Matendo 2:2-4
5
Matendo 2:46-47
Siku zote kwa moyo mmoja walikutana ndani ya ukumbi wa Hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba, wakila chakula chao kwa furaha na moyo mweupe, wakimsifu Mwenyezi Mungu na kuwapendeza watu wote. Kila siku Bwana Mwenyezi akawaongeza waumini wale waliokuwa wakiokolewa.
Explore Matendo 2:46-47
6
Matendo 2:17
“ ‘Katika siku za mwisho, asema Mungu, nitamimina Roho wangu juu ya wote wenye mwili. Wana wenu na binti zenu watatabiri, vijana wenu wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
Explore Matendo 2:17
7
Matendo 2:44-45
Walioamini wote walikuwa mahali pamoja, nao walikuwa na kila kitu shirika. Waliuza mali zao na vitu walivyokuwa navyo, kila mtu akagawiwa kadiri ya mahitaji yake.
Explore Matendo 2:44-45
8
Matendo 2:21
Na kila mtu atakayeliitia jina la Bwana Mwenyezi Mungu, ataokolewa.’
Explore Matendo 2:21
9
Matendo 2:20
Jua litakuwa giza na mwezi utakuwa mwekundu kama damu, kabla ya kuja siku ile kuu ya Mwenyezi Mungu iliyo tukufu.
Explore Matendo 2:20
Home
Bible
Plans
Videos