1
2 Wafalme 6:17
Biblia Habari Njema
Kisha Elisha akaomba, “Ee Mwenyezi-Mungu, umfumbue macho ili apate kuona!” Basi, Mwenyezi-Mungu akamfumbua macho huyo kijana, akaona farasi na magari ya moto yakiwa kila mahali katika mlima wote, kumzunguka Elisha.
Compare
Explore 2 Wafalme 6:17
2
2 Wafalme 6:16
Elisha akamjibu, “Usiogope kwa sababu walio pamoja nasi ni wengi kuliko walio pamoja nao.”
Explore 2 Wafalme 6:16
3
2 Wafalme 6:15
Mtumishi wa Elisha alipoamka mapema kesho yake na kutoka nje, akaona jeshi pamoja na farasi na magari ya kukokotwa limeuzingira mji. Akarudi ndani akasema, “Ole wetu, ee, Bwana wangu! Sasa tutafanya nini?”
Explore 2 Wafalme 6:15
4
2 Wafalme 6:18
Waaramu waliposhambulia, Elisha alimwomba Mwenyezi-Mungu akisema, “Nakuomba uwafanye watu hawa wawe vipofu!” Mwenyezi-Mungu akasikiliza ombi lake na kuwafanya vipofu.
Explore 2 Wafalme 6:18
5
2 Wafalme 6:6
Elisha akauliza, “Liliangukia wapi?” Mtu huyo akamwonesha. Elisha akakata kijiti na kukitupa majini na papo hapo shoka likaelea juu ya maji.
Explore 2 Wafalme 6:6
6
2 Wafalme 6:5
Mmoja wao alipokuwa anakata miti, shoka lake likachomoka na kuanguka majini; akalia, akisema, “Sasa bwana wangu nitafanya nini? Shoka hili tulikuwa tumeliazima!”
Explore 2 Wafalme 6:5
7
2 Wafalme 6:7
Elisha akamwamuru alichukue naye akanyosha mkono, akalichukua.
Explore 2 Wafalme 6:7
Home
Bible
Plans
Videos