1
Isaya 30:21
Biblia Habari Njema
Mkienda kulia au kushoto, mtasikia sauti nyuma yenu ikisema, “Njia ni hii; ifuateni.”
Compare
Explore Isaya 30:21
2
Isaya 30:18
Hata hivyo, Mwenyezi-Mungu anangoja awafadhili, atainuka na kuwaonea huruma. Maana, Mwenyezi-Mungu ni Mungu atendaye haki. Heri wote wale wanaomtumainia.
Explore Isaya 30:18
3
Isaya 30:15
Bwana Mungu, Mtakatifu wa Israeli, asema: “Mkinirudia na kutulia mtaokolewa; kwa utulivu na kunitumainia mtapata nguvu.” Lakini nyinyi hamkutaka.
Explore Isaya 30:15
4
Isaya 30:20
Ingawa Bwana atawalisha taabu na kuwanywesha dhiki, yeye ndiye Mwalimu wenu na hatajificha tena; nanyi mtamwona kwa macho yenu wenyewe.
Explore Isaya 30:20
5
Isaya 30:19
Enyi watu wa Siyoni, enyi watu wa Yerusalemu, hakika nyinyi hamtaomboleza tena. Kweli Mungu atawahurumia; mara tu atakaposikia kilio chenu atawaitikeni.
Explore Isaya 30:19
6
Isaya 30:1
Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Ole wao watoto wanaoniasi, wanaotekeleza mipango yao na si mipango yangu, wanaofanya mikataba kinyume cha matakwa yangu! Naam, wanarundika dhambi juu ya dhambi.
Explore Isaya 30:1
Home
Bible
Plans
Videos