Nani awezaye kupima maji ya bahari kwa konzi yake,
kuzipima mbingu kwa mikono yake?
Nani awezaye kuutia udongo wa dunia kikombeni;
kuipima milima kwa mizani
au vilima kwa kipimo cha uzani?
Nani awezaye kuiongoza akili ya Mwenyezi-Mungu,
au kuwa mshauri wake na kumfunza?
Mwenyezi-Mungu alimtaka nani shauri,
ndipo akapata kuwa mwenye ujuzi?
Nani aliyemfunza njia za haki?
Nani aliyemfundisha maarifa,
na kumwonesha namna ya kuwa na akili?