1
Isaya 42:6-7
Biblia Habari Njema
“Mimi Mwenyezi-Mungu nimekuita kutenda haki, nimekushika mkono na kukulinda. Kwa njia yako nitaweka ahadi na watu wote, wewe utakuwa mwanga wa mataifa. Utayafumbua macho ya vipofu, utawatoa wafungwa gerezani, waliokaa gizani utawaletea uhuru.
Compare
Explore Isaya 42:6-7
2
Isaya 42:8
Jina langu mimi ni Mwenyezi-Mungu; utukufu wangu sitampa mwingine, wala sifa zangu sanamu za miungu.
Explore Isaya 42:8
3
Isaya 42:1
“Tazameni mtumishi wangu ninayemtegemeza; mteule wangu ambaye moyo wangu umependezwa naye. Nimeiweka roho yangu juu yake, naye atayaletea mataifa haki.
Explore Isaya 42:1
4
Isaya 42:3-4
Mwanzi uliochubuka hatauvunja, utambi ufukao moshi hatauzima; ataleta haki kwa uaminifu. Yeye hatafifia wala kufa moyo, hata atakapoimarisha haki duniani. Watu wa mbali wanangojea mwongozo wake.”
Explore Isaya 42:3-4
5
Isaya 42:16
“Nitawaongoza vipofu katika njia wasiyoifahamu, nitawaongoza katika njia ambazo hawazijui. Mbele yao giza nitaligeuza kuwa mwanga, na mahali pa kuparuza patakuwa laini. Huo ndio mpango wangu wa kufanya, nami nitautekeleza.
Explore Isaya 42:16
6
Isaya 42:9
Tazama, mambo niliyotabiri yametukia; na sasa natangaza mambo mapya, nakueleza hayo kabla hayajatukia.”
Explore Isaya 42:9
Home
Bible
Plans
Videos