1
Isaya 6:8
Biblia Habari Njema
Kisha nikamsikia Mwenyezi-Mungu akisema, “Nimtume nani? Ni nani atakayekuwa mjumbe wetu?” Nami nikajibu, “Niko hapa! Nitume mimi.”
Compare
Explore Isaya 6:8
2
Isaya 6:3
Waliitana kila mmoja na mwenzake hivi: “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, ni Mwenyezi-Mungu wa majeshi! Dunia yote imejaa utukufu wake.”
Explore Isaya 6:3
3
Isaya 6:5
Basi, mimi nikasema, “Ole wangu! Mimi nimeangamia, maana, midomo yangu ni najisi, na watu ninaoishi nao ni najisi kama mimi. Hata hivyo, kwa macho yangu mwenyewe, nimemwona Mfalme, Mwenyezi-Mungu wa majeshi.”
Explore Isaya 6:5
4
Isaya 6:1
Mnamo mwaka aliofariki mfalme Uzia, nilimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi kilicho juu na cha fahari. Pindo la vazi lake lilienea hekaluni mote
Explore Isaya 6:1
5
Isaya 6:7
Naye akinigusa nalo mdomoni, akasema: “Tazama, kaa hili limekugusa mdomo; umeondolewa hatia yako, umesamehewa dhambi yako.”
Explore Isaya 6:7
6
Isaya 6:2
na juu yake walikuwa wamekaa malaika. Kila mmoja alikuwa na mabawa sita: Mawili ya kufunika uso, mawili ya kufunika mwili na mawili ya kurukia.
Explore Isaya 6:2
7
Isaya 6:6
Basi, mmoja wa hao malaika akaruka kunijia, akiwa ameshika mkononi koleo lililokuwa na kaa la moto alilolitwaa madhabahuni.
Explore Isaya 6:6
8
Isaya 6:9
Naye akaniambia, “Nenda ukawaambie watu hawa: ‘Mtasikiliza sana, lakini hamtaelewa; mtatazama sana, lakini hamtaona.’”
Explore Isaya 6:9
9
Isaya 6:10
Kisha akaniambia, “Zipumbaze akili za watu hawa, masikio yao yasisikie, macho yao yasione; ili wasije wakaona kwa macho yao, wakasikia kwa masikio yao, wakaelewa kwa akili zao, na kunigeukia, nao wakaponywa.”
Explore Isaya 6:10
Home
Bible
Plans
Videos