Kila ninaposema kitu, nalalamika,
napaza sauti, “Ukatili na uharibifu!”
Maana kwangu kutangaza neno la Mwenyezi-Mungu
kwanifanya nishutumiwe na kudhihakiwa kutwa nzima.
Lakini nikisema, “Sitamtaja Mwenyezi-Mungu,
wala sitasema tena kwa jina lake,”
moyoni mwangu huwa na kitu kama moto uwakao,
uliofungiwa ndani ya mifupa yangu.
Najaribu sana kuuzuia humo,
lakini ninashindwa.