Mungu huongea na watu katika ndoto na maono,
wakati usingizi mzito unapowavamia,
wanaposinzia vitandani mwao.
Hapo huwafungulia watu masikio yao;
huwatia hofu kwa maonyo yake,
wapate kuachana na matendo yao mabaya,
na kuvunjilia mbali kiburi chao.
Hivyo humkinga mtu asiangamie shimoni,
maisha yake yasiangamie kwa upanga.