1
Methali 11:25
Biblia Habari Njema
Mtu mkarimu atafanikishwa, amnyweshaye mwingine maji naye atanyweshwa.
Compare
Explore Methali 11:25
2
Methali 11:24
Atoaye kwa ukarimu huzidi kutajirika; lakini bahili huzidi kudidimia katika umaskini.
Explore Methali 11:24
3
Methali 11:2
Kiburi huandamana na fedheha, lakini kwa watu wanyenyekevu mna hekima.
Explore Methali 11:2
4
Methali 11:14
Pasipo na uongozi taifa huanguka, penye washauri wengi pana usalama.
Explore Methali 11:14
5
Methali 11:30
Matendo ya mwadilifu huleta uhai, lakini uhalifu huuondoa uhai.
Explore Methali 11:30
6
Methali 11:13
Apitapitaye akichongea hutoa siri, lakini anayeaminika rohoni huficha siri.
Explore Methali 11:13
7
Methali 11:17
Mtu mkarimu hufaidika yeye mwenyewe, lakini mtu mkatili hujiumiza mwenyewe.
Explore Methali 11:17
8
Methali 11:28
Anayetegemea mali zake ataanguka, lakini mwadilifu atastawi kama jani bichi.
Explore Methali 11:28
9
Methali 11:4
Utajiri haufai kitu siku ya ghadhabu, lakini uadilifu huokoa kutoka kifo.
Explore Methali 11:4
10
Methali 11:3
Unyofu wa watu wema huwaongoza, upotovu wa wenye hila huwaangamiza.
Explore Methali 11:3
11
Methali 11:22
Mwanamke mzuri asiye na akili, ni kama pete ya dhahabu puani mwa nguruwe.
Explore Methali 11:22
12
Methali 11:1
Mizani ya udanganyifu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, lakini matumizi ya kipimo halali ni furaha kwake.
Explore Methali 11:1
Home
Bible
Plans
Videos