YouVersion Logo
Search Icon

Waebrania 1

1
Mwenyezi Mungu amesema kupitia Mwana
1Zamani, Mungu alisema na baba zetu kupitia kwa manabii mara nyingi na kwa njia mbalimbali, 2lakini katika siku hizi za mwisho anasema nasi kupitia kwa Mwanawe, ambaye amemweka kuwa mrithi wa vitu vyote, na ambaye kupitia kwake aliuumba ulimwengu. 3Mwana ni mng’ao wa utukufu wa Mungu na mfano halisi wa nafsi yake, akivihifadhi vitu vyote kwa neno lake lenye uweza. Baada ya kufanya utakaso kwa ajili ya dhambi, aliketi mkono wa kuume wa Aliye Mkuu huko mbinguni. 4Kwa hiyo alifanyika bora kuliko malaika, kama jina alilorithi lilivyo bora kuliko lao.
Mwana ni mkuu kuliko malaika
5Kwa maana ni kwa malaika yupi Mungu aliwahi kusema,
“Wewe ni Mwanangu;
leo mimi nimekuwa Baba yako”#1:5 Zaburi 2:7?
Au tena,
“Mimi nitakuwa Baba yake,
naye atakuwa Mwanangu”#1:5 2 Samweli 7:14; 1 Nyakati 17:13?
6Tena, Mungu amletapo mzaliwa wake wa kwanza ulimwenguni, anasema,
“Malaika wote wa Mungu na wamsujudu.”#1:6 Kumbukumbu 32:43
7Anaponena kuhusu malaika, anasema,
“Huwafanya malaika wake kuwa pepo,
watumishi wake kuwa miali ya moto.”#1:7 Zaburi 104:4
8Lakini kwa habari za Mwana asema,
“Kiti chako cha enzi, Ee Mungu,
kitadumu milele na milele,
nayo haki itakuwa fimbo ya utawala
ya ufalme wako.
9Umependa haki na kuchukia uovu;
kwa hiyo Mungu, Mungu wako,
amekuweka juu ya wenzako
kwa kukupaka mafuta ya furaha.”#1:9 Zaburi 45:6, 7
10Pia asema,
“Hapo mwanzo, Ee Mwenyezi Mungu,
uliweka misingi ya dunia,
nazo mbingu ni kazi ya mikono yako.
11Hizo zitatoweka, lakini wewe utadumu;
zote zitachakaa kama vazi.
12Utazikunjakunja kama joho,
nazo zitabadilishwa kama vazi.
Lakini wewe hubadiliki,
nayo miaka yako haikomi kamwe.”#1:12 Zaburi 102:25-27
13Je, ni kwa malaika yupi Mungu aliwahi kusema,
“Keti mkono wangu wa kuume,
hadi nitakapowaweka adui zako
chini ya miguu yako”#1:13 Zaburi 110:1?
14Je, malaika wote si roho watumikao, waliotumwa kuwahudumia wale watakaourithi wokovu?

Currently Selected:

Waebrania 1: NENO

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in