YouVersion Logo
Search Icon

Yona 2

2
Maombi Ya Yona Katika Tumbo La Nyangumi
1Akiwa ndani ya tumbo la nyangumi, Yona alimwomba Bwana Mungu wake. 2 Akasema:
“Katika shida yangu nalimwita Bwana,
naye akanijibu.
Kutoka kina cha kaburi#2:2 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol. niliomba msaada,
nawe ukasikiliza kilio changu.
3 Ulinitupa kwenye kilindi,
ndani kabisa ya moyo wa bahari,
mikondo ya maji ilinizunguka,
mawimbi yako yote na viwimbi
vilipita juu yangu.
4 Nikasema, ‘Nimefukuziwa
mbali na uso wako,
hata hivyo nitatazama tena
kuelekea Hekalu lako takatifu.’
5 Maji yaliyonimeza yalinitisha,
kilindi kilinizunguka;
mwani#2:5 Mwani hapa maana yake ni magugu yaotayo kwenye sakafu ya kilindi cha bahari. ulijisokota kichwani pangu.
6 Nilizama chini sana mpaka pande za mwisho za milima,
makomeo ya hiyo nchi yalinifungia hata milele.
Lakini uliuleta uhai wangu kutoka shimoni,
Ee Bwana Mungu wangu.
7 “Wakati uhai wangu ulipokuwa unatoka,
nilikukumbuka wewe, Bwana,
nayo maombi yangu yalikufikia wewe,
katika Hekalu lako takatifu.
8 “Wale watu wanaongʼangʼana na sanamu zisizofaa
hupoteza neema ile ambayo ingekuwa yao.
9 Lakini mimi, kwa wimbo wa shukrani,
nitakutolea dhabihu.
Lile nililowekea nadhiri nitalitimiza.
Wokovu watoka kwa Bwana.”
10 Basi Bwana akamwamuru yule nyangumi, naye akamtapika Yona katika nchi kavu.

Currently Selected:

Yona 2: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in