YouVersion Logo
Search Icon

Mathayo Utangulizi

Utangulizi
Mathayo alikuwa mtoza ushuru ambaye Bwana Yesu alimwita awe mwanafunzi wake hapo mwanzoni mwa huduma yake ya hadharani. Mathayo alianza Injili yake kwa kueleza kwa kirefu kuhusu Yesu alivyozaliwa na bikira Maria, alivyobatizwa, na kujaribiwa nyikani. Yesu alikuja akihubiri kuhusu Ufalme wa Mungu, ambao ni wa kila mtu anayetaka kupata uzima wa milele. Mtu anaingia katika Ufalme huu kwa kutubu dhambi na kumwamini Yesu. Mathayo aliyagawa mafundisho ya Yesu katika sehemu kuu tano: Maadili, Kueneza Habari Njema, Mifano, Ushirika, na Kuja kwa Ufalme wa Mungu. Sehemu ya Mwisho ya Injili ya Mathayo inaeleza juu ya kufa na kufufuka kwa Yesu, na agizo alilolitoa kwa wote wanaomwamini kueneza Habari Njema ulimwenguni kote.
Mwandishi
Mathayo aitwaye Lawi.
Kusudi
Kumtambulisha Yesu kwa Wayahudi kuwa ndiye Masiya, na pia Mfalme wa milele.
Mahali
Palestina.
Tarehe
Kati ya 60–65 B.K.
Wahusika Wakuu
Yesu na wanafunzi wake, Maria, Yohana Mbatizaji na wanafunzi wake, viongozi wa dini ya Kiyahudi, na Pilato.
Wazo Kuu
Kudhibitisha kwamba Bwana Yesu alikamilisha ahadi ambazo Mungu alitoa katika Agano la Kale.
Mambo Muhimu
Kitabu hiki kinaelezea matukio manne ya utoto wa Yesu. Pia kinapeana mifano kumi aliyoitoa Yesu, na miujiza miwili aliyoifanya. Ina midahalo tisa ambayo Yesu alihojiana na baadhi ya watu. Kinamalizia na hisia sita zilizoandamana na kusulubiwa kwake, na maagizo kwa wanafunzi wake kueneza Habari Njema duniani kote.
Mgawanyo
Maisha na huduma ya Bwana Yesu (1:1–4:25)
Mahubiri ya Mlimani (5:1–7:29)
Mafundisho ya mifano na mazungumzo (8:1–18:35)
Safari ya kwenda Yerusalemu, na maonyo ya mwisho (19:1–23:39)
Unabii kuhusu mambo yajayo (24:1–25:46)
Kufa na kufufuka kwa Bwana Yesu (26:1–28:20).

Currently Selected:

Mathayo Utangulizi: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in