YouVersion Logo
Search Icon

Marko Utangulizi

Utangulizi
Yohana Marko, mwandishi wa Injili hii, alitajwa na mababa wa Jumuiya ya kwanza ya waumini wa Isa, yaani Papiasi, Irenio na Klementi wa Iskanderia, kuwa mshirika wa karibu sana wa Mtume Petro. Yohana Marko alikuwa mtoto wa Mariamu, ambaye nyumba yake ilikuwa kituo kikuu cha Jumuiya ya waumini wa Isa huko Yerusalemu. Hatimaye Marko aliishi Rumi ambako aliandika kumbukumbu za Mtume Petro.
Marko alisafiri na mjomba wake, Barnaba, hadi Antiokia ya Siria walipofuatana na Paulo kwenye safari yake ya kwanza kueneza Injili. Hata hivyo, Marko aliwaacha Barnaba na Paulo huko Kipro na kurudi Yerusalemu. Baadaye Barnaba na Marko walielekea Kipro wakati Paulo alienda jimbo la Asia. Miaka kama kumi baadaye, Marko alikuwa pamoja na Paulo huko Rumi. Shabaha ya Marko ilikuwa kukusanya pamoja ujumbe wote wa Injili ya Al-Masihi kwa kifupi.
Mwandishi
Yohana Marko.
Kusudi
Kumtambulisha Isa, kazi, na mafundisho yake.
Mahali
Rumi.
Tarehe
Mnamo 55–65 B.K.
Wahusika Wakuu
Isa Al-Masihi na wanafunzi wake, Pilato, na viongozi wa dini ya Kiyahudi.
Wazo Kuu
Marko anamdhihirisha Bwana Isa kuwa Mtumishi wa Mwenyezi Mungu, na Mtu wa vitendo aliyekuja kuyatimiza mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
Mambo Muhimu
Marko anaanza kwa kueleza habari za huduma ya Bwana Isa hadharani na mahubiri yake kuhusu Habari Njema za ufalme wa Mwenyezi Mungu. Kisha anatoa wazi unabii kuhusu matazamio ya kifo cha Bwana Isa. Hatimaye anaeleza jinsi Bwana Isa alivyosulubiwa msalabani kwa ajili ya dhambi za ulimwengu, na alivyofufuliwa kutoka kwa wafu; pia maneno na maagizo yake ya mwisho kwa wanafunzi wake.
Yaliyomo
Huduma ya Yahya (1:1-13)
Huduma ya Isa huko Galilaya (1:14–9:50)
Safari ya kwenda Yerusalemu na matukio mjini (10:1–12:44)
Unabii kuhusu mambo yajayo (13:1-37)
Kufa na kufufuka kwa Isa (14:1–16:20).

Currently Selected:

Marko Utangulizi: NENO

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in