YouVersion Logo
Search Icon

Mithali Utangulizi

Utangulizi
Neno la Kiebrania ni “Mashal”; ndilo lililotafsiriwa “Mithali” na lina maana nyingine zaidi, yaani “Mapokeo,” “Mafumbo,” au “Semi za hekima.” Hivyo Mithali ni mkusanyiko wa semi nyingi za hekima, na mambo kuhusu maisha ya busara na haki ya kila siku. Kitabu hiki kinatoa mafundisho yenye mafumbo ambayo yalikuwa ya kawaida katika eneo la Mashariki ya Kati ya zamani. Hekima yake ni ya kipekee kwa sababu imeelezwa katika mtazamo wa Mungu na viegezo vyake vya haki kwa ajili ya watu wake wa Agano. Kama vile Daudi alivyo chimbuko la Zaburi katika Israeli, ndivyo Solomoni alivyo chimbuko la hekima katika Israeli (1:1; 10:1; 25:1).
Mwandishi
Solomoni, Aguri mwana wa Yake, Mfalme Lemueli, na wenye hekima ambao majina yao hayakutajwa; zilikusanywa pamoja na Mfalme Hezekia.
Kusudi
Kusudi la kitabu hiki ni kuwafundisha watu jinsi ya kupata hekima, adabu njema na maisha ya uadilifu, jinsi ya kufanya vitu katika njia sahihi na ya haki, na njia inayompendeza Mungu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Zilikusanywa pamoja na Mfalme Hezekia kati ya 715–686 K.K.
Wahusika Wakuu
Solomoni, Aguri na Lemueli.
Wazo Kuu
Kumjua Mungu ndio mwanzo wa hekima.
Mambo Muhimu
Kati ya mambo muhimu ambayo yameorodheshwa katika kitabu hiki ni: Vijana na nidhamu, familia, kumjua Mungu, ndoa, kufahamu ukweli na hekima.
Mgawanyo
Maelezo juu ya hekima na upumbavu (1:1–9:18)
Mithali za Solomoni (10:1–22:16)
Mithali za wengine wenye hekima (22:17–24:34)
Mithali nyingine za Solomoni (25:1–29:27)
Mithali za Aguri na Lemueli (30:1–31:31).

Currently Selected:

Mithali Utangulizi: NEN

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in