YouVersion Logo
Search Icon

Yer 47

47
Hukumu juu ya Wafilisti
1 # Isa 14:29-31; Eze 25:15-17; Yoe 3:4-8; Amo 1:6-8; Sef Neno la BWANA lililomjia Yeremia, nabii, katika habari za Wafilisti, kabla Farao hajapiga Gaza. 2:4-7; Zek 9:5-7
2 # Isa 8:7; Yer 1:14 BWANA asema hivi, Tazama, maji yanatokea katika pande za kaskazini, nayo yatakuwa mto ufurikao, nayo yataifunika nchi, na kila kitu kilichomo, huo mji na wote wakaao ndani yake; nao watu watalia na watu wote wakaao katika nchi watapiga yowe. 3#Nah 3:2Kwa sababu ya mshindo wa kukanyaga kwato za farasi wake walio hodari, kwa sababu ya mwendo wa mbiombio wa magari yake ya vita; kwa sababu ya ngurumo ya magurudumu yake, hao akina baba hawatazami nyuma ili kuwaangalia watoto wao, kwa kuwa mikono yao ni dhaifu; 4#Yer 25:22; Yoe 3:4; Amo 1:9,10; 9:7; Mwa 10:14kwa sababu ya siku ijayo kuwaangamiza Wafilisti wote, kukatilia mbali kila msaidizi wa Tiro na Sidoni asaliaye; maana BWANA atawaharibu Wafilisti, mabaki ya kisiwa cha Kaftori.
5 # Sef 2:4 Upaa umeupata Gaza;
Ashkeloni umenyamazishwa
Mabaki ya bonde lao;
Hata lini utajikata-kata?
6 # Eze 21:3 Ee upanga wa BWANA,
Siku ngapi zitapita kabla hujatulia?
Ujitie katika ala yako;
Pumzika, utulie.
7 # 1 Sam 3:12; Mik 6:9 Utawezaje kutulia,
Ikiwa BWANA amekupa agizo?
Juu ya Ashkeloni na juu ya pwani,
Ndipo alipoyaamuru hayo.

Currently Selected:

Yer 47: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in