YouVersion Logo
Search Icon

Yos 13

13
Sehemu za Kanaani ambazo Hazijatekwa
1 # Mwa 18:11; Yos 14:10; 24:29; 1 Fal 1:1; Lk 1:7 Basi Yoshua alipokuwa mzee, na kwendelea sana miaka yake, BWANA akamwambia, Wewe umekuwa mzee na kwendelea sana miaka yako, kisha inasalia nchi nyingi sana bado kumilikiwa. 2#Kut 23:29,31; Kum 11:23,24; Amu 3:1; Mwa 10:14; 26:1; Yoe 3:4; 1 Sam 27:8; 2 Sam 3:3Nchi iliyosalia ni hii; nchi zote za Wafilisti, na Wageshuri wote; 3#Yer 2:18; 1 Sam 6:4,16; Sef 2:5; Kum 2:23kutoka Shihori, hicho kijito kilichokabili Misri, hata mpaka wa Ekroni upande wa kaskazini, nchi inayohesabiwa kuwa ni ya hao Wakanaani; mashehe matano wa hao Wafilisti; Wagaza, na Waashdodi, na Waashkeloni, na Wagiti, na Waekroni; tena Waavi, 4#Yos 19:30; Amu 1:34upande wa kusini; nchi yote ya Wakanaani na Meara iliyo ya Wasidoni, mpaka Afeka, hata mpaka wa Waamori; 5#1 Fal 5:18; Zab 83:7; Eze 27:9; Yos 12:7na nchi ya Wagebali na Lebanoni yote, upande wa kuelekea maawio ya jua, kutoka Baal-gadi ulio chini ya mlima wa Hermoni mpaka kufikilia maingilio ya Hamathi; 6#Hes 33:54; Yos 11:8; 23:13; Amu 2:21; Yos 14:1,2na watu wote wenye kuikaa nchi ya vilima kutoka Lebanoni hata Misrefoth-maimu, maana, hao Wasidoni wote; hao wote nitawafukuza watoke mbele ya wana wa Israeli; lakini wewe uwape Israeli kuwa ni urithi wao, kama nilivyokuamuru. 7Basi sasa gawanya nchi hii, iwe urithi wa hizi kabila kenda, na nusu ya kabila ya Manase.
Nchi iliyo Mashariki mwa Yordani
8 # Hes 32:33; Kum 3:12; Yos 22:4 Pamoja na yeye, Wareubeni na Wagadi walipata urithi wao, waliopewa na Musa, huko ng’ambo ya Yordani upande wa mashariki, vile vile kama huyo Musa mtumishi wa BWANA alivyowapa; 9#Hes 21:30; Isa 15:2; Yer 48:18,22kutoka huko Aroeri, iliyo pale ukingoni mwa bonde la Amoni, na huo mji ulio pale katikati ya bonde, na nchi tambarare yote ya Medeba mpaka Diboni; 10na miji yote ya Sihoni mfalme wa Waamori, aliyetawala katika Heshboni, hata mpaka wa wana wa Amoni; 11#Yos 12:5na Gileadi na mpaka wa Wageshuri, na Wamaaka, na mlima wa Hermoni wote, na Bashani yote mpaka Saleka; 12#Kum 3:11; Hes 21:24ufalme wote wa Ogu uliokuwa katika Bashani, huyo aliyekuwa akitawala katika Ashtarothi na katika Edrei (huyo alisalia katika mabaki ya wale Warefai); kwa kuwa Musa aliwapiga hao na kuwafukuza. 13Pamoja na hayo wana wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri, wala Wamaaka; lakini Wageshuri na Wamaaka wamekaa kati ya Israeli, hata siku hii ya leo. 14#Kum 18:1; 10:9; 12:12,19; Hes 18:20; Yos 14:3,4Lakini hakuwapa watu wa kabila ya Lawi urithi uwao wote; maana sadaka za BWANA, Mungu wa Israeli, zisongezwazo kwa njia ya moto ndizo urithi wake huyo, kama alivyomwambia.
Nchi ya Reubeni
15Musa akawapa kabila ya wana wa Reubeni kwa kadiri ya jamaa zao. 16#Hes 21:28,30; Kum 3:12; Yos 12:2Mpaka wao ulikuwa kutoka hapo Aroeri, iliyo pale ukingoni mwa bonde la Arnoni, na huo mji ulio katikati ya bonde, na nchi tambarare yote iliyo karibu na Medeba; 17na Heshboni na miji yake yote iliyoko katika bonde; na Diboni, na Bamoth-baali, na Beth-baal-meoni; 18#Hes 21:23na Yahasa, na Kedemothi, na Mefaathi; 19#Hes 32:37na Kiriathaimu, na Sibma, na Sereth-shahari katika kilima cha hilo bonde; 20na Beth-peori, na nchi za matelemko ya Pisga, na Beth-yeshimothi; 21#Kum 3:10; Hes 21:24; 31:8na miji yote ya nchi tambarare, na ufalme wote wa Sihoni mfalme wa Waamori, aliyekuwa akitawala katika Heshboni, aliyepigwa na Musa pamoja na hao wakubwa wa Midiani, nao ni Evi, na Rekemu, na Suri, na Huri, na Reba, hao mashehe wa Sihoni, waliokuwa katika nchi hiyo. 22#Hes 22:5; 24:1; 31:8; 2 Pet 2:15; Ufu 2:14Balaamu naye, huyo mwana wa Beori, huyo mchawi, wana wa Israeli walimwua kwa upanga kati ya hao wengine waliowaua.
23Na mpaka wa wana wa Reubeni ulikuwa ni mto wa Yordani, na mpaka wake. Huo ndio urithi wa wana wa Reubeni sawasawa na jamaa zao, miji yake na vijiji vyake.
Nchi ya Gadi
24Musa akawapa kabila ya Gadi, hao wana wa Gadi, kwa kadiri ya jamaa zao. 25#Hes 32:35; 21:26-29; Kum 2:19; Amu 11:13; 2 Sam 11:1; 12:26Mpaka wao ulikuwa ni Yazeri, na miji hiyo ya Gileadi, na nusu ya nchi ya wana wa Amoni, mpaka Aroeri uliokabili Raba; 26tena kutoka Heshboni mpaka Ramath-Mizpe, na Betonimu; tena kutoka Mahanaimu hata mpaka wa Debiri; 27#Mwa 33:17; 1 Fal 7:46; Hes 34:11; Kum 3:17; Yos 11:2; Mt 14:34; Lk 5:1tena katika bonde, Beth-haramu, na Bethnimira, na Sukothi, na Safoni, hiyo iliyosalia ya ufalme wa Sihoni mfalme wa Heshboni, yaani mto wa Yordani na mpaka wake, mpaka mwisho wa bahari ya Kinerethi ng’ambo ya pili ya Yordani upande wa mashariki. 28Huo ndio urithi wa wana wa Gadi sawasawa na jamaa zao, miji yake na vijiji vyake.
Nchi ya Nusu Kabila la Manase (Mashariki)
29Kisha Musa akawapa hao wa nusu ya kabila ya Manase urithi wao; ulikuwa ni wa hiyo nusu ya kabila ya wana wa Manase sawasawa na jamaa zao. 30#Hes 32:41; 1 Nya 2:23Na mpaka wao ulikuwa kutoka huko Mahanaimu, Bashani yote, na ufalme wote wa Ogu mfalme wa Bashani, na miji yote ya Yairi, iliyo katika Bashani, miji sitini; 31#Yos 12:4na nusu ya Gileadi, na Ashtarothi, na Edrei, hiyo miji ya ufalme wa Ogu katika Bashani, ilikuwa ni ya wana wa Makiri mwana wa Manase maana, kwa hiyo nusu ya wana wa Makiri sawasawa na jamaa zao.
32Hizi ndizo mirathi ambazo Musa alizigawanya katika nchi tambarare za Moabu, ng’ambo ya pili ya Yordani, kukabili Yeriko, upande wa mashariki. 33#Hes 18:20; Yos 18:7; Kum 10:9; 12:12; 14:27,29; 18:1,2; Eze 44:28Lakini Musa hakuwapa kabila ya Lawi urithi uwao wote; yeye BWANA, Mungu wa Israeli, ndiye urithi wao, kama alivyowaambia.

Currently Selected:

Yos 13: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in