YouVersion Logo
Search Icon

Mt 2

2
Wageni kutoka Mashariki
1 # Lk 2:1-7 Yesu alipozaliwa katika Bethlehemu ya Uyahudi zamani za mfalme Herode, tazama, mamajusi wa mashariki walifika Yerusalemu, wakisema, 2#Hes 24:17Yuko wapi yeye aliyezaliwa mfalme wa Wayahudi? Kwa maana tuliiona nyota yake mashariki, nasi tumekuja kumsujudia. 3Basi mfalme Herode aliposikia hayo, alifadhaika, na Yerusalemu pia pamoja naye. 4Akakusanya wakuu wa makuhani wote na waandishi wa watu, akatafuta habari kwao, Kristo azaliwa wapi? 5#Mik 5:2; Yn 7:42Nao wakamwambia, Katika Bethlehemu ya Uyahudi; kwa maana ndivyo ilivyoandikwa na nabii,
6 # Mik 5:1 Nawe Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,
Hu mdogo kamwe katika majumbe wa Yuda;
Kwa kuwa kwako atatoka mtawala
Atakayewachunga watu wangu Israeli.
7Kisha Herode akawaita wale mamajusi faraghani, akapata kwao hakika ya muda tangu ilipoonekana ile nyota. 8Akawapeleka Bethlehemu, akasema, Shikeni njia, mkaulize sana mambo ya mtoto; na mkiisha kumwona, nileteeni habari, ili mimi nami niende nimsujudie. 9Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto. 10Nao walipoiona ile nyota, walifurahi furaha kubwa mno. 11#Zab 72:10,15; Isa 60:6Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane. 12Nao wakiisha kuonywa na Mungu katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.
Yusufu Akimbilia Misri
13 # Kut 2:15 Na hao walipokwisha kwenda zao, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto, akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukae huko hata nikuambie; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize. 14Akaondoka akamchukua mtoto na mama yake usiku, akaenda zake Misri; 15#Hos 11:1akakaa huko hata alipokufa Herode; ili litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema,
Kutoka Misri nalimwita mwanangu.
Mauaji ya Watoto Wachanga
16Ndipo Herode, alipoona ya kuwa amedhihakiwa na wale mamajusi, alighadhabika sana, akatuma watu akawaua watoto wote wanaume waliokuwako huko Bethlehemu na viungani mwake mwote, tangu wenye miaka miwili na waliopungua, kwa muda ule aliouhakikisha kwa wale mamajusi. 17#Yer 31:15Ndipo lilipotimia neno lililonenwa na nabii Yeremia, akisema,
18 # Yer 31:15; Mwa 35:19 Sauti ilisikiwa Rama,
Kilio, na maombolezo mengi,
Raheli akiwalilia watoto wake,
Asikubali kufarijiwa, kwa kuwa hawako.
Yusufu Arudi kutoka Misri
19Hata alipofariki Herode, tazama, malaika wa Bwana alimtokea Yusufu katika ndoto huko Misri, 20#Kut 4:19akasema, Ondoka, umchukue mtoto na mamaye, ushike njia kwenda nchi ya Israeli; kwa maana wamekufa walioitafuta roho ya mtoto. 21Akaondoka akamchukua mtoto na mamaye, akafika nchi ya Israeli. 22Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki huko Uyahudi mahali pa Herode babaye, aliogopa kwenda huko; naye akiisha kuonywa katika ndoto, akasafiri pande za Galilaya, 23#Mk 1:24; Lk 1:26; 2:39; Yn 1:45; Isa 11:1; 53:2akaenda, akakaa katika mji ulioitwa Nazareti; ili litimie neno lililonenwa na manabii, Ataitwa Mnazorayo.

Currently Selected:

Mt 2: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in