6
Kuhusu Utoaji Sadaka
1 #
Mt 23:5
Angalieni msifanye wema wenu machoni pa watu, kusudi mtazamwe na wao; kwa maana mkifanya kama hayo, hampati thawabu kwa Baba yenu aliye mbinguni.
2Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na watu. 3#Mt 25:37-40; Rum 12:8Amin, nawaambieni, Wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; 4sadaka yako iwe kwa siri; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Kuhusu Maombi
5 #
Lk 18:10-14; Mt 23:5,6 Tena msalipo, msiwe kama wanafiki; kwa maana wao wapenda kusali hali wamesimama katika masinagogi na katika pembe za njia, ili waonekane na watu. Amin, nawaambia, Wamekwisha kupata thawabu yao. 6#2 Fal 4:33Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
7 #
Isa 1:15
Nanyi mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. 8#Mt 6:32Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba. 9#Lk 11:2-4; Yn 17:6Basi ninyi salini hivi;
Baba yetu uliye mbinguni,
Jina lako litukuzwe,
Ufalme wako uje,
10 #
Mt 7:21; Lk 22:42 Mapenzi yako yatimizwe,
hapa duniani kama huko mbinguni.
11Utupe leo riziki yetu.
12 #
Mt 14:15; 18:21-35 Utusamehe deni zetu,
kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu.
13 #
1 Nya 29:11-13; Yn 17:11,15 Na usitutie majaribuni,
lakini utuokoe na yule mwovu.
[Kwa kuwa ufalme ni wako, na nguvu, na utukufu, hata milele.
Amina.]
14 #
Mk 11:25-26
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. 15Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.
Kuhusu Kufunga
16 #
Isa 58:5-9
Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao. 17Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso; 18ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.
Kuhusu Hazina
19 #
Yak 5:2-3
Msijiwekee hazina duniani, nondo na kutu viharibupo, na wevi huvunja na kuiba; 20#Mt 19:21; Lk 12:33,34; Kol 3:1,2bali jiwekeeni hazina mbinguni, kusikoharibika kitu kwa nondo wala kutu, wala wevi hawavunji wala hawaibi; 21kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
Jicho Kamili
22 #
Lk 11:34-36
Taa ya mwili ni jicho; basi jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru. 23#Mt 20:15Lakini jicho lako likiwa bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Basi ile nuru iliyomo ndani yako ikiwa giza; si giza hilo!
Kutumikia Mabwana Wawili
24 #
Lk 16:9,13 Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali.
Msisumbuke
25 #
Lk 12:22-31
#
Flp 4:6; 1 Pet 5:7; 1 Tim 6:6; Ebr 13:5 Kwa sababu hiyo nawaambieni, Msisumbukie maisha yenu, mle nini au mnywe nini; wala miili yenu, mvae nini. Maisha je! Si zaidi ya chakula, na mwili zaidi ya mavazi?
26 #
Mt 10:29-31
Waangalieni ndege wa angani, ya kwamba hawapandi, wala hawavuni, wala hawakusanyi ghalani; na Baba yenu wa mbinguni huwalisha hao. Ninyi je! Si bora kupita hao? 27Ni yupi kwenu ambaye akijisumbua aweza kujiongeza kimo chake hata mkono mmoja? 28Na mavazi, ya nini kuyasumbukia? Fikirini maua ya mashamba, jinsi yameavyo; hayafanyi kazi, wala hayasokoti 29#1 Fal 10:4-7; 2 Nya 9:3-6nami nawaambia, ya kwamba hata Sulemani katika fahari yake yote hakuvikwa vizuri kama mojawapo la hayo. 30Basi, ikiwa Mungu huyavika hivi majani ya kondeni, yaliyopo leo, na kesho hutupwa kalibuni, je! Hatazidi sana kuwavika ninyi, enyi wa imani haba? 31Msisumbuke, basi, mkisema, Tule nini? Au Tunywe nini? Au Tuvae nini? 32#Mt 6:8Kwa maana hayo yote Mataifa huyatafuta; kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua ya kuwa mnahitaji hayo yote. 33#Rum 14:17; 1 Fal 3:13,14; Zab 37:4,25Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. 34#Kut 16:19Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.