YouVersion Logo
Search Icon

Mit 12

12
1Kila apendaye mafundisho hupenda maarifa;
Bali yeye achukiaye kulaumiwa ni kama mnyama.
2Mtu mwema atapata upendeleo kwa BWANA;
Bali mtu wa hila atahukumiwa naye.
3Mtu hatathibitika kwa njia ya uovu;
Shina la mwenye haki halitaondolewa kamwe.
4 # Mit 31:23; 1 Kor 11:7; Mit 14:30 Mwanamke mwema ni taji ya mumewe;
Bali aaibishaye ni kama kuoza mifupani mwake.
5Mawazo ya mwenye haki ni adili;
Bali mashauri ya mtu mwovu ni hadaa.
6Maneno ya waovu huotea damu;
Bali kinywa cha wanyofu kitawaokoa.
7 # Mt 7:24 Waovu huangamia, hata hawako tena;
Bali nyumba ya mwenye haki itasimama.
8 # 1 Sam 13:13; Mal 2:8,9; Mit 1:25,26; 3:35; Mt 27:4,5 Mtu atasifiwa kwa kadiri ya akili zake;
Bali mwenye moyo wa ukaidi atadharauliwa.
9Afadhali mtu anayedharauliwa, ikiwa ana mtumwa,
Kuliko ajisifuye, ikiwa anahitaji chakula.
10 # Kum 25:4 Mwenye haki huufikiri uhai wa mnyama wake;
Bali huruma za mtu mwovu ni ukatili.
11 # Mwa 3:19; Mit 28:19; Efe 4:28; 1 The 4:11 Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele;
Bali afuataye mambo ya upuzi hana ufahamu.
12 # Zab 1:3; Lk 8:15 Asiye haki hutamani nyavu za wabaya;
Bali shina lao wenye haki huleta matunda.
13 # 2 Pet 2:9 Katika kosa la midomo kuna mtego kwa mbaya;
Bali mwenye haki atatoka katika taabu.
14 # Isa 3:10 Mtu atashiba mema kwa matunda ya kinywa chake;
Na atarudishiwa matendo ya mikono yake.
15 # Lk 18:11 Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe;
Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.
16Ghadhabu ya mpumbavu hujulika mara;
Bali mtu mwerevu husitiri aibu.
17Atamkaye maneno ya kweli hufunua haki;
Bali shahidi wa uongo hutamka hila.
18Kuna anenaye bila kufikiri, kama kuchoma kwa upanga;
Bali ulimi wa mwenye haki ni afya.
19 # Zek 1:5,6 Mdomo wa kweli utathibitishwa milele;
Bali ulimi wa uongo ni wa kitambo tu.
20Hila imo mioyoni mwao wafikirio uovu;
Bali wafanyao mashauri ya amani, kwao kuna furaha.
21 # Rum 8:28; 2 The 1:6; 2 Pet 2:9 Mwenye haki hatapatikana na msiba wo wote;
Bali wasio haki watajazwa mabaya.
22 # Ufu 22:15 Midomo ya uongo ni chukizo kwa BWANA;
Bali watendao uaminifu ndio furaha yake.
23Mwanadamu mwenye busara husitiri maarifa;
Bali moyo wa wapumbavu hutangaza upumbavu.
24 # 1 Fal 11:28; Mit 10:4 Mkono wa mwenye bidii utatawala;
Bali mvivu atalipishwa kodi.
25 # Isa 50:4 Uzito katika moyo wa mtu huuinamisha;
Bali neno jema huufurahisha.
26Mwenye haki ni kiongozi cha mwenzake;
Bali njia ya wasio haki huwakosesha.
27Mtu mvivu hapiki mawindo yake;
Bali mwenye bidii anazo mali za thamani.
28 # Kum 30:15; Mt 19:17; Rum 5:21; 2 Kor 4:17; Ufu 2:7 Katika njia ya haki kuna uhai;
Wala hakuna mauti katika mapito yake.

Currently Selected:

Mit 12: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in