YouVersion Logo
Search Icon

Zab 131

131
Kumtumainia Mungu kwa Utulivu
Wimbo wa kupanda mlima.
1 # Rum 12:16 BWANA, moyo wangu hauna kiburi,
Wala macho yangu hayainuki.
Wala sijishughulishi na mambo makuu,
Wala na mambo yashindayo nguvu zangu.
2 # Mt 18:3 Hakika nimeituliza nafsi yangu,
Na kuinyamazisha.
Kama mtoto aliyeachishwa
Kifuani mwa mama yake;
Kama mtoto aliyeachishwa,
Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu.
3Ee Israeli, umtarajie BWANA,
Tangu leo na hata milele.

Currently Selected:

Zab 131: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in