68
Sifa na Shukrani
Kwa mwimbishaji. Ya Daudi. Zaburi. Wimbo.
1Mungu huondoka, adui zake wakatawanyika,
Nao wamchukiao huukimbia uso wake.
2Kama moshi upeperushwavyo,
Ndivyo uwapeperushavyo wao;
Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto,
Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu.
3Bali wenye haki hufurahi,
Na kuushangilia uso wa Mungu,
Naam, hupiga kelele kwa furaha.
4Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake,
Mtengenezeeni njia ya barabara,
Apitaye majangwani kama mpanda farasi;
Jina lake ni YAHU; shangilieni mbele zake.
5Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane,
Mungu katika kao lake takatifu.
6 #
1 Sam 2:5
Mungu huwakalisha wapweke nyumbani;
Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa;
Bali wakaidi hukaa katika nchi kavu.
7 #
Hab 3:13
Ee Mungu, ulipotoka mbele ya watu wako,
Ulipopita nyikani,
8 #
Kut 19:18
Nchi ilitetemeka
Naam, mbingu zilidondoka usoni pa Mungu;
Hata Sinai usoni pa Mungu; Mungu wa Israeli.
9Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema;
Urithi wako ulipochoka uliutia nguvu.
10 #
Zab 74:19
Kabila yako ilifanya kao lake huko;
Ee Mungu, kwa wema wako uliwaruzuku walioonewa.
11Bwana analitoa neno lake;
Wanawake watangazao habari ni jeshi kubwa;
12Wafalme wa majeshi wanakimbia, wanakimbia;
Na mwanamke akaaye nyumbani agawa nyara.
13 #
Zab 81:6; Efe 5:26,27 Kwa nini kulala mazizini arukapo hua,
Mbawa zake ziking’aa kama fedha
Na manyoya yake kama dhahabu?
14Mwenyezi Mungu alipotawanya wafalme huko,
Kulinyesha theluji katika Salmoni.
15Ni mlima wa Mungu mlima Bashani,
Ni mlima mrefu mlima Bashani.
16Enyi milima mirefu, kwani kuutazama kwa wivu
Mlima alioutamani Mungu akae juu yake?
Naam, BWANA atakaa juu yake milele.
17 #
Kum 33:2; 2 Fal 6:17; Dan 7:10 Magari ya Mungu ni ishirini elfu, maelfu maelfu;
Bwana yumo kati yao kama katika Sinai,
Katika patakatifu.
18 #
Amu 5:12; Zab 78:60; Mdo 1:9; 2:4; Efe 4:8; 1 Tim 1:13 Wewe umepaa juu, umeteka mateka,
Umepewa vipawa katikati ya wanadamu;
Naam, hata na wakaidi, BWANA Mungu akae nao.
19Na ahimidiwe Bwana,
Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu;
Mungu ndiye wokovu wetu.
20 #
Kum 32:39
Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa;
Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana.
21Naam, Mungu atakipasua kichwa cha adui zake,
Utosi wenye nywele wa mtu afulizaye kukosa.
22Bwana alisema, Kutoka Bashani nitawarudisha,
Nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari;
23Uuchovye mguu wako katika damu ya adui zako,
Na ulimi wa mbwa zako upate sehemu yake.
24Ee Mungu, wameiona miendo yako;
Miendo ya Mungu wangu, Mfalme wangu, katika patakatifu
25Waimbaji hutangulia, nyuma yao wapigao vinanda,
Kati ya wanawali wapiga matari.
26Mhimidini Mungu katika mikutano,
Bwana katika makusanyiko ya Israeli.
27Yuko Benyamini mdogo, mtawala wao;
Wakuu wa Yuda, kundi lao;
Wakuu wa Zabuloni;
Wakuu wa Naftali.
28Ee Mungu, uziamuru nguvu zako;
Ee Mungu, uwe hodari uliyetufanyia makuu.
29 #
2 Nya 32:23; Isa 60:16 Kwa ajili ya hekalu lako Yerusalemu
Wafalme watakuletea hedaya.
30Mkemee mnyama wa manyasini;
Kundi la mafahali, na ndama za watu;
Hata wanyenyekee na kuleta vipande vya fedha,
Uwatawanye watu wapendao vita.
31 #
Isa 19:19; 45:14; Sef 3:10; Mdo 8:27,28 Masheki watakuja kutoka Misri,
Kushi itamnyoshea Mungu mikono yake mara.
32Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu,
Msifuni Bwana kwa nyimbo.
33Apandaye mbingu za mbingu za tangu milele;
Aitoa sauti yake, sauti ya nguvu.
34Mhesabieni Mungu nguvu;
Enzi yake i juu ya Israeli;
Na nguvu zake zi mawinguni.
35 #
Isa 41:10; Zek 10:12; Yn 15:5; Efe 6:10; Flp 4:13 Mungu ni mwenye kutisha
Kutoka patakatifu pako.
Ndiye Mungu wa Israeli;
Yeye huwapa watu wake nguvu na uwezo.
Na ahimidiwe Mungu.