YouVersion Logo
Search Icon

Zab 95

95
Mwito wa Kuabudu na Kutii
1Njoni, tumwimbie BWANA,
Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.
2Tuje mbele zake kwa shukrani,
Tumfanyie shangwe kwa zaburi.
3Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu,
Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.
4Mkononi mwake zimo bonde za dunia,
Hata vilele vya milima ni vyake.
5Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya,
Na mikono yake iliumba nchi kavu.
6 # 1 Fal 8:54; 1 Nya 6:13; Ezr 9:5; Dan 6:10; Lk 22:41; Mdo 7:60; 1 Kor 6:20; Efe 3:14; Ayu 35:10; Isa 54:5; Yn 1:3 Njoni, tuabudu, tusujudu,
Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.
7 # Ebr 3:15; 4:7; Ebr 3:7-11; Ebr 3:7-11; Hes 14:22 Kwa maana ndiye Mungu wetu,
Na sisi tu watu wa malisho yake,
Na kondoo za mkono wake.
Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
8 # Kut 17:1-7; Hes 20:2-13 Msifanye migumu mioyo yenu;
Kama vile huko Meriba
Kama siku ya Masa jangwani.
9Hapo waliponijaribu baba zenu,
Wakanipima, wakayaona matendo yangu.
10 # Ebr 3:10 Miaka arobaini nalihuzunika na kizazi kile,
Nikasema, Hao ni watu waliopotoka mioyo,
Hawakuzijua njia zangu.
11 # Hes 14:20-23; Kum 1:34-36; 12:9-10; Ebr 4:3,5 Nikaapa kwa hasira yangu
Wasiingie rahani mwangu.

Currently Selected:

Zab 95: SUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in