15
Pendezeni Wengine wala sio Kujipendeza wenyewe
1Basi imetupasa sisi tulio na nguvu kuuchukua udhaifu wao wasio na nguvu, wala haitupasi kujipendeza wenyewe. 2#1 Kor 9:19; 10:24,33Kila mtu miongoni mwetu na ampendeze jirani yake, apate wema, akajengwe. 3#Zab 69:9Kwa maana Kristo naye hakujipendeza mwenyewe; bali kama ilivyoandikwa, Malaumu yao waliokulaumu wewe yalinipata mimi. 4#Rum 4:23,24; 1 Kor 10:11Kwa kuwa yote yaliyotangulia kuandikwa yaliandikwa ili kutufundisha sisi; ili kwa saburi na faraja ya maandiko tupate kuwa na tumaini. 5#Flp 3:16Na Mungu mwenye saburi na faraja awajalie kunia mamoja ninyi kwa ninyi, kwa mfano wa Kristo Yesu; 6ili kwa moyo mmoja na kwa kinywa kimoja mpate kumtukuza Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo.
Injili kwa Wayahudi na Wamataifa
7Kwa hiyo mkaribishane ninyi kwa ninyi, kama naye Kristo alivyotukaribisha, ili Mungu atukuzwe. 8#Mt 15:24; Mdo 3:25Kwa maana nasema, ya kwamba Kristo amefanyika mhudumu wa agano la kutahiriwa kwa ajili ya kweli ya Mungu, kusudi azithibitishe ahadi walizopewa baba zetu; 9#2 Sam 22:50; Zab 18:49; Rum 11:30tena ili Mataifa wamtukuze Mungu kwa ajili ya rehema zake; kama ilivyoandikwa,
Kwa hiyo nitakushukuru kati ya Mataifa,
Nami nitaliimbia jina lako.
10 #
Kum 32:43
Na tena anena,
Furahini, Mataifa, pamoja na watu wake.
11 #
Zab 117:1
Na tena,
Enyi Mataifa yote, msifuni Bwana;
Enyi watu wote, mhimidini.
12 #
Isa 11:10; Ufu 5:5 Na tena Isaya anena,
Litakuwako shina la Yese,
Naye aondokeaye kuwatawala Mataifa;
Ndiye Mataifa watakayemtumaini.
13Basi Mungu wa tumaini na awajaze ninyi furaha yote na amani katika kuamini, mpate kuzidi sana kuwa na tumaini, katika nguvu za Roho Mtakatifu.
Sababu ya Paulo kuwa Bayana
14Ndugu zangu, nimehakikishwa mimi mwenyewe kwa habari zenu ya kuwa ninyi nanyi mmejaa wema, mmejazwa elimu yote, tena mwaweza kuonyana. 15#Rum 1:5; 12:3Lakini nawaandikia, kwa ujasiri zaidi katika sehemu za waraka huu, kana kwamba kuwakumbusha, kwa neema ile niliyopewa na Mungu, 16#Rum 11:13; Flp 2:17ili niwe mhudumu wa Kristo Yesu kati ya watu wa Mataifa, niifanyie Injili ya Mungu kazi ya ukuhani, kusudi Mataifa wawe sadaka yenye kibali, ikiisha kutakaswa na Roho Mtakatifu. 17Basi, nina sababu ya kuona fahari katika Kristo Yesu mbele za Mungu. 18#2 Kor 3:5Maana sitathubutu kutaja neno asilolitenda Kristo kwa kazi yangu, Mataifa wapate kutii, kwa neno au kwa tendo, 19#Mk 16:17kwa nguvu za ishara na maajabu, katika nguvu za Roho Mtakatifu; hata ikawa tangu Yerusalemu, na kando kando yake, mpaka Iliriko nimekwisha kuihubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu; 20#2 Kor 10:15,16kadhalika nikijitahidi kuihubiri Injili, nisihubiri hapo ambapo jina la Kristo limekwisha kutajwa, nisije nikajenga juu ya msingi wa mtu mwingine; 21#Isa 52:15bali kama ilivyoandikwa,
Wale wasiohubiriwa habari zake wataona,
Na wale wasiojasikia watafahamu.
Mpango wa Paulo Kuutembelea Rumi
22 #
Rum 1:10-13
Ndiyo sababu nalizuiwa mara nyingi nisije kwenu. 23Lakini sasa, kwa kuwa sina wasaa tena pande hizi, tena tangu miaka mingi nina shauku kuja kwenu; 24#1 Kor 16:6wakati wo wote nitakaosafiri kwenda Spania [nitakuja kwenu.] Kwa maana nataraji kuwaona ninyi katika kusafiri kwangu, na kusafirishwa nanyi, moyo wangu ushibe kwenu kidogo. 25#1 Kor 16:1-4#Mdo 19:21; 20:22Ila sasa ninakwenda Yerusalemu, nikiwahudumu watakatifu; 26#1 Kor 16:1; 2 Kor 8:1; 9:2,12maana imewapendeza watu wa Makedonia na Akaya kufanya changizo kwa ajili ya watakatifu huko Yerusalemu walio maskini. 27#1 Kor 9:11; Rum 9:4Naam, imewapendeza, tena wamekuwa wadeni wao. Kwa maana ikiwa Mataifa wameyashiriki mambo yao ya roho, imewabidi kuwahudumu kwa mambo yao ya mwili. 28Basi nikiisha kuimaliza kazi hiyo, na kuwatilia muhuri tunda hilo, nitapitia kwenu, kwenda Spania. 29#Rum 1:11Nami najua ya kuwa nikija kwenu nitakuja kwa utimilifu wa baraka ya Kristo.
30 #
2 Kor 1:11; Flp 1:27; Kol 4:3; 2 The 3:1 Ndugu zangu, nawasihi kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kwa upendo wa Roho, jitahidini pamoja nami katika maombi yenu kwa ajili yangu mbele za Mungu; 31kwamba niokolewe na wale wasioamini katika Uyahudi, na tena huduma yangu niliyo nayo huko Yerusalemu ikubalike kwa watakatifu; 32nipate kufika kwenu kwa furaha, kama apendavyo Mungu, nikapate kupumzika pamoja nanyi. 33Mungu wa amani na awe pamoja nanyi nyote. Amina.