2
Toa Mafundisho Mema
1 #
1 Tim 6:3; 2 Tim 1:13 Lakini wewe nena mambo yapasayo mafundisho yenye uzima; 2#1 Tim 5:1ya kwamba wazee wawe wenye kiasi, wastahivu, wenye busara, wazima katika imani na katika upendo na katika saburi. 3#1 Tim 3:11Vivyo hivyo na wazee wa kike wawe na mwenendo wa utakatifu; wasiwe wasingiziaji, wasiwe wenye kutumia mvinyo nyingi, bali wafundishao mema; 4ili wawatie wanawake vijana akili, wawapende waume zao, na kuwapenda watoto wao; 5#Efe 5:22na kuwa wenye kiasi, kuwa safi, kufanya kazi nyumbani mwao, kuwa wema, kuwatii waume zao wenyewe; ili neno la Mungu lisitukanwe.
6Vivyo hivyo na vijana waume uwaonye kuwa na kiasi; 7#1 Tim 4:12; 1 Pet 5:3katika mambo yote ukijionyesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionyesha usahihi na ustahivu, 8#1 Pet 2:15na maneno yenye uzima yasiyoweza kuhukumiwa makosa, ili yule mwenye kupinga atahayarike, kwa kuwa hana neno baya la kunena juu yetu.
9 #
Efe 6:5; 1 Tim 6:1; 1 Pet 2:18 Watumwa na wawatii bwana zao, wakiwapendeza katika mambo yote; wasiwe wenye kujibu, 10#Tit 1:3wasiwe waibaji; bali wauonyeshe uaminifu mwema wote, ili wayapambe mafundisho ya Mwokozi wetu Mungu katika mambo yote. 11Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; 12#Efe 1:4; 1 Yoh 2:16nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; 13#1 Kor 1:7; Rum 5:2; Flp 3:20tukilitazamia tumaini lenye baraka na mafunuo ya utukufu wa Kristo Yesu, Mungu mkuu na Mwokozi wetu; 14#Kut 19:5; Kum 4:20; 7:6; 14:2; Zab 130:8; 1 Pet 2:9; 3:13; Gal 1:4; 1 Tim 2:6; Efe 2:10; Eze 37:23ambaye alijitoa nafsi yake kwa ajili yetu, ili atukomboe na maasi yote, na kujisafishia watu wawe milki yake mwenyewe, wale walio na juhudi katika matendo mema.
15 #
1 Tim 4:12
Nena maneno hayo, onya na kukaripia kwa mamlaka yote; asikudharau mtu awaye yote.