Matendo 4
4
Petro na Yohana mbele ya baraza
1 #
Lk 22:4,52 Hata walipokuwa wakisema na watu wale, makuhani na walinzi wa hekalu na Masadukayo wakawatokea, 2#Mdo 23:8 wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuhubiri kuwa katika Yesu kuna ufufuo wa wafu. 3#Mdo 3:1 Wakawakamata, wakawaweka gerezani hadi asubuhi; kwa kuwa imekwisha kuwa jioni. 4#Mdo 2:47 Lakini wengi katika hao waliosikia lile neno waliamini; na hesabu ya wanaume ikawa kama elfu tano.
5Kesho yake, wakubwa na wazee na waandishi wakakusanyika Yerusalemu, 6na Anasi Kuhani Mkuu, na Kayafa pia, na Yohana na Iskanda, na wote wale waliokuwa jamaa zake Kuhani Mkuu. 7#Mt 21:23 Walipowaweka katikati wakawauliza, Kwa nguvu gani na kwa jina la nani ninyi mmefanya haya? 8#Mt 10:19,20 Ndipo Petro, akijaa Roho Mtakatifu, akawaambia, Enyi wakubwa wa watu na wazee wa Israeli, 9kama tukiulizwa leo habari ya jambo jema alilofanyiwa yule mtu dhaifu, jinsi alivyoponywa, 10#Mdo 3:6,13-16 jueni ninyi nyote na watu wote wa Israeli ya kuwa kwa jina la Yesu Kristo wa Nazareti, ambaye ninyi mlimsulubisha, na Mungu akamfufua katika wafu, kwa jina hilo mtu huyu anasimama akiwa mzima mbele yenu. 11#Zab 118:22; Mt 21:42 Yeye ndiye jiwe lile lililodharauliwa na ninyi waashi, nalo limewekwa kuwa jiwe kuu la pembeni. 12#Mt 1:21 Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
13Basi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kuwajua ya kuwa ni watu wasio na elimu, wasio na maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu. 14#Mdo 3:8,9 Na wakimwona yule aliyeponywa akisimama pamoja nao hawakuwa na neno la kujibu. 15Wakawaamuru kutoka katika baraza, wakashauriana wao kwa wao, 16#Yn 11:47 wakisema, Tuwafanyie nini watu hawa? Maana ni dhahiri kwa watu wote wakaao Yerusalemu ya kwamba ishara mashuhuri imefanywa nao, wala hatuwezi kuikana. 17#Mdo 5:28 Lakini ili neno hili lisije likaenea katika watu, na tuwatishe wasiseme tena na mtu yeyote kwa jina hili. 18Wakawaita, wakawaamuru wasiseme kabisa wala kufundisha kwa jina la Yesu. 19#Mdo 5:29 Petro na Yohana wakawajibu wakawaambia, Kama ni haki mbele za Mungu kuwasikiliza ninyi kuliko Mungu, hukumuni ninyi wenyewe; 20maana sisi hatuwezi kuacha kuyanena mambo tuliyoyaona na kuyasikia. 21Nao walipokwisha kuwatisha tena wakawafungua, wasione njia ya kuwaadhibu, kwa sababu ya watu; kwa kuwa watu wote walikuwa wakimtukuza Mungu kwa hayo yaliyotendeka; 22maana umri wake yule mtu aliyefanyiwa ishara hii ya kuponya ulipita miaka arubaini.
Waumini waomba wawe na ujasiri
23Hata walipofunguliwa, wakaenda kwa watu wao, wakawapasha habari ya mambo yote waliyoambiwa na wakuu wa makuhani na wazee. 24#Kut 20:11; Neh 9:6; Zab 146:6; Isa 37:16; Lk 2:29; Ufu 6:10 Nao waliposikia, wakampazia Mungu sauti zao kwa moyo mmoja, wakisema, Mola, wewe ndiwe Mungu, ndiwe uliyefanya mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo; 25#Zab 2:1-2 nawe ulinena kwa Roho Mtakatifu kwa kinywa cha baba yetu Daudi, mtumishi wako,
Mbona mataifa wamefanya ghasia,
Na makabila wametafakari ubatili?
26Wafalme wa dunia wamejipanga,
Na wakuu wameshauriana pamoja
Juu ya Bwana na juu ya Kristo wake.
27 #
Mt 27:1-2; Mk 15:1; Lk 23:1,7-11; Yn 18:28-29 Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta, 28#Mdo 2:23 ili wafanye yote ambayo mkono wako na mashauri yako yamekusudia tangu zamani yatokee. 29#Efe 6:19 Basi sasa, Bwana, viangalie vitisho vyao; ukawajalie watumwa wako kunena neno lako kwa ujasiri wote, 30ukinyosha mkono wako kuponya; ishara na maajabu vifanyike kwa jina la Mtumishi wako mtakatifu Yesu. 31#Mdo 2:2,4 Hata walipokwisha kumwomba Mungu, mahali pale walipokusanyika pakatikiswa, wote wakajaa Roho Mtakatifu, wakanena neno la Mungu kwa ujasiri.
Waumini washiriki mali zao pamoja
32 #
Mdo 2:44-45
Na jamii ya watu walioamini walikuwa na moyo mmoja na roho moja; wala hapana mmoja aliyesema ya kuwa kitu chochote alicho nacho ni mali yake mwenyewe; bali walimiliki vitu vyote kwa pamoja. 33#Mdo 2:47 Na mitume wakatoa ushuhuda wa kufufuka kwake Yesu kwa nguvu nyingi, na neema nyingi ikawa juu yao wote. 34#Mdo 2:45 Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji; kwa sababu watu wote waliokuwa na viwanja au nyumba waliviuza, wakaileta thamani ya vitu vile vilivyouzwa, 35wakaiweka miguuni pa mitume; kila mtu akagawiwa kwa kadiri ya alivyohitaji.
36 #
Mdo 11:22,24; 13:4; 15:39 Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro, 37alikuwa na shamba akaliuza, akaileta fedha, akaiweka miguuni pa mitume.
Currently Selected:
Matendo 4: SRUVDC
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: