YouVersion Logo
Search Icon

1 Petro 3

3
Wake na waume
1 # Efe 5:22; Kol 3:18; Tit 2:5 Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 2#1 Pet 2:12 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. 3#1 Tim 2:9; Isa 3:18-24 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; 4bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. 5Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. 6#Mwa 18:12; Mit 3:25 Kama vile Sara alivyomtii Abrahamu, akamwita bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, pasipo kutishwa na hofu yoyote. 7#Efe 5:25; Kol 3:19 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; maana wao pia ni warithi wa neema ya uzima, ili maombi yenu yasizuiliwe na chochote.
Mateso kwa ajili ya kutenda Haki
8 # Rum 12:16 Neno la mwisho ni hili; muwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; 9#Zab 34:12-16; Yak 1:26; Mt 5:44; 1 The 5:15; 1 Pet 2:23 watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka. 10#Zab 34:12-16; Yak 1:26 Kwa maana,
Atakaye kupenda maisha,
Na kuona siku njema,
Auzuie ulimi wake usinene mabaya,
Na midomo yake isiseme uongo.
11Na aache mabaya, atende mema;
Atafute amani, aifuate sana.
12Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki,
Na masikio yake husikiliza maombi yao;
Bali uso wa Bwana uko juu ya watenda mabaya.
13Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema? 14#Mt 5:10; Isa 8:12-13; 1 Pet 2:20 Lakini hata mkiteswa kwa sababu ya kutenda haki, mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu. 15#Isa 8:13; Kol 4:6; 1 Pet 1:3,13 Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa heshima. 16#1 Pet 2:12 Nanyi muwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo. 17#1 Pet 2:20-24 Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya. 18#Rum 6:10; Efe 2:18; Ebr 9:28; 10:10 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; akauawa kimwili, lakini akahuishwa kiroho, 19#1 Pet 4:8 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiria; 20#Mwa 6:1—7:7,17,24 watu wasiotii hapo zamani, wakati Mungu alipowavumilia kwa subira, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji. 21#Efe 5:26; Ebr 10:22 Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. 22#Efe 1:20,21; Zab 110:1; Kol 1:16 Naye yuko katika mkono wa kulia wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.

Currently Selected:

1 Petro 3: SRUV

Highlight

Share

Copy

None

Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in