Danieli 3
3
Sanamu ya dhahabu
1 #
1 Fal 12:28; Zab 96:5; Isa 41:24; Hos 2:8; 1 Kor 8:4 Nebukadneza, mfalme, alifanya sanamu ya dhahabu, ambayo urefu wake ulikuwa ni dhiraa sitini, na upana wake dhiraa sita; akaisimamisha katika uwanda wa Dura, katika wilaya ya Babeli. 2Ndipo Nebukadneza akatuma watu kuwakusanya maamiri, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, majaji, mahakimu na wakuu wa wilaya zote, ili wahudhurie wakati wa kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha. 3#Mt 7:13; Mdo 19:34,35; Rum 1:20,23 Ndipo maamiri, wasimamizi, watawala, washauri, watunza hazina, majaji, mahakimu na wakuu wa wilaya zote, wakakusanyika ili kuizindua ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha; wakasimama mbele ya ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha. 4#Dan 4:1 Ndipo mpiga mbiu akapiga kelele akisema, Enyi watu wa kabila zote, na taifa, na lugha, mmeamriwa hivi, 5wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zumari, na namna zote za ngoma, lazima kuanguka na kuiabudu sanamu ya dhahabu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha. 6#Yer 29:22; Ufu 13:15 Na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa saa iyo hiyo katika tanuri liwakalo moto. 7Basi wakati huo, watu wa kabila zote walipoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zumari, na namna zote za ngoma, watu wote na mataifa na lugha wakaanguka, wakaiabudu ile sanamu, mfalme Nebukadneza aliyoisimamisha.
8 #
Dan 6:12; Est 3:6; Ezr 4:12-16 Basi baadhi ya Wakaldayo wakakaribia, wakaleta mashitaka juu ya Wayahudi. 9#Neh 2:3; Hos 7:3; Dan 2:4; 5:10 Wakajibu, wakamwambia mfalme Nebukadneza, Ee mfalme, uishi milele. 10Wewe, Ee mfalme, ulitoa amri ya kwamba kila mtu atakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zumari, na namna zote za ngoma, ni lazima aanguke na kuiabudu ile sanamu ya dhahabu; 11na kila mtu asiyeanguka na kuabudu atatupwa katika tanuri liwakalo moto. 12#Est 3:8; Dan 2:49 Wako Wayahudi kadha wa kadha uliowaweka juu ya mambo ya wilaya ya Babeli, yaani, Shadraka, na Meshaki, na Abednego; watu hawa, Ee mfalme, hawakukujali wewe; hawaitumikii miungu yako, wala kuiabudu ile sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha. 13#Mt 10:18; Mk 13:9; Mdo 5:25-27 Basi Nebukadneza akatoa amri kwa hasira na ghadhabu, waletwe hao Shadraka, na Meshaki, na Abednego. Basi wakawaleta watu hao mbele ya mfalme. 14#Isa 46:1 Nebukadneza akajibu, akawaambia, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, je! Ni kwa makusudi hata hamumtumikii mungu wangu wala kuisujudia sanamu ya dhahabu niliyoisimamisha? 15#Kut 32:32; 5:2; Lk 13:9; 2 Fal 18:35 Basi sasa, kama mkiwa tayari wakati mtakapoisikia sauti ya panda, na filimbi, na kinubi, na zeze, na santuri, na zumari, na namna zote za ngoma, kuanguka na kuisujudia sanamu niliyoisimamisha, ni vema; bali msipoisujudia, mtatupwa saa iyo hiyo katika tanuri liwakalo moto; naye ni nani Mungu yule atakayewaokoa ninyi mikononi mwangu? 16#Mt 10:19; Mdo 26:24 Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakajibu, wakamwambia mfalme, Ee Nebukadneza, hamna haja kukujibu katika neno hili. 17#1 Sam 17:37; Mik 7:7; 2 Kor 1:10 Kama ni hivyo, Mungu wetu tunayemtumikia aweza kutuokoa na tanuri liwakalo moto; naye atatuokoa mkononi mwako, Ee mfalme. 18#Mt 10:32; Ebr 11:25 Bali kama si hivyo, ujue, Ee mfalme, ya kuwa sisi hatukubali kuitumikia miungu yako, wala kuisujudia hiyo sanamu ya dhahabu uliyoisimamisha.
Tanuri liwakalo
19Ndipo Nebukadneza akajaa ghadhabu, na sura ya uso wake ikabadilika juu ya Shadraka, na Meshaki, na Abednego, basi akatoa amri watie moto ile tanuri mara saba kuliko desturi yake ya kutiwa moto. 20Kisha akawaamuru baadhi ya watu mashujaa wa jeshi lake kuwafunga Shadraka, na Meshaki, na Abednego, na kuwatupa katika lile tanuri lililokuwa likiwaka moto. 21Basi watu hao wakafungwa, wakiwa wamevaa suruali zao, na kanzu zao, na majoho yao, na mavazi yao mengine, wakatupwa katikati ya lile tanuri lililokuwa likiwaka moto. 22Basi kwa sababu amri ya mfalme ilikuwa ni kali, na lile tanuri lilikuwa lina moto sana, mwako wa ule moto ukawaua wale watu waliowashika Shadraka, na Meshaki, na Abednego. 23#Zab 33:18; 40:4; Isa 43:2; 2 Kor 1:8-10; 1 Pet 4:12 Na watu hao watatu, Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakaanguka, wakiwa wamefungwa, katikati ya lile tanuri lililokuwa linawaka moto.
24Ndipo Nebukadneza akastaajabu, akainuka kwa haraka; akanena, akawaambia mawaziri wake, Je! Hatukutupa watu watatu, wakiwa wamefungwa, katikati ya moto? Wakajibu, wakamwambia mfalme, Kweli, Ee mfalme. 25#Isa 43:2; Ayu 1:6; Zab 34:7; Yn 19:7; Ebr 1:14 Akajibu, akasema, Tazama, mimi naona watu wanne, nao wamefunguliwa, wanatembea katikati ya moto hali hawana dhara; na sura yake yule wa nne ni mfano wa mwana wa miungu. 26Kisha Nebukadneza akaukaribia mlango wa lile tanuri lililokuwa linawaka moto. Akanena, akasema, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye Juu, tokeni, mje huku. Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakatoka katika ule moto. 27#Mk 16:18; Ebr 11:34 Na maamiri, wasimamizi, watawala, na mahakimu, waliokuwa wamekusanyika pamoja, wakawaona watu hao, ya kuwa ule moto ulikuwa hauna nguvu juu ya miili yao, wala nywele za vichwa vyao hazikuteketea, wala suruali zao hazikubadilika, wala harufu ya moto haikuwapata hata kidogo. 28#1 Nya 5:20; Zab 34:7,8; Efe 1:12,13; 1 Pet 1:21 Nebukadneza akanena, akasema, Na ahimidiwe Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego; aliyemtuma malaika wake, akawaokoa watumishi wake waliomtumaini, wakaligeuza neno la mfalme, na kujitoa miili yao ili wasimtumikie mungu mwingine, wala kumwabudu, ila Mungu wao wenyewe. 29#Kum 32:31; Zab 3:8; Dan 6:27 Basi mimi naweka amri ya kuwa kila kabila la watu, na kila taifa, na kila lugha, watakaonena neno lolote lisilopasa juu ya huyo Mungu wa Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watakatwa vipande vipande, na nyumba zao zitafanywa jaa; kwa kuwa hakuna Mungu mwingine awezaye kuokoa namna hii. 30Kisha mfalme akawakuza Shadraka, na Meshaki, na Abednego, katika wilaya ya Babeli.
Currently Selected:
Danieli 3: SRUV
Highlight
Share
Copy
Want to have your highlights saved across all your devices? Sign up or sign in
Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.

: